×

Rais Samia Ampokea Rais wa Namibia, Dk Netumbo Nandi-Ndaitwah, Ikulu Dar (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Namibia Dkt, Netumbo Nandi-Ndaitwah baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa Ziara ya Kitaifa, tarehe 20 Juni, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amempokea Rais wa Jamhuri ya Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah aliyewasili nchini kwa ziara ya kitaifa leo Juni 20, 2026.

Hafla ya mapokezi imefanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha zaidi uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia.

Mapokezi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na ujumbe waandamizi kutoka pande zote mbili, ambapo nchi hizo zinatarajiwa kujadili na kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali za maendeleo.

Rais Dkt. Samia akiwa amesimama na mgeni wake Rais Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah wakati wakipokea heshima ya Wimbo wa Taifa katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar.
Rais Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah akikagua Gwaride la Heshima la Mapokezi katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar.
Rais Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah akiangalia vikundi vya ngoma za asili baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kikwete, Ikulu Jijini Dar.
Rais Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar.

Leave a Comment