×

Serikali Yachukua Ushauri wa Aziza Sleyum, Miradi 6 Mikubwa ya Barabara Kutekelezwa kwa PPP

Ikiwa ni siku chache tu tangu Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Aziza Sleyum Ally, achangie mjadala wa Bajeti ya Serikali bungeni na kusisitiza umuhimu wa mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), akiishauri serikali kuutumia mfumo huo kuchochea ukuaji wa uchumi katika sekta za barabara, maji na afya, sasa ushauri wake umeanza kuzaa matunda.

Hatua hiyo imejidhihirisha baada ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kutangaza fursa za uwekezaji katika miradi sita mikubwa ya kimkakati ya barabara kuu kupitia mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).

Miradi hiyo ya kihistoria ni pamoja na upanuzi wa Barabara ya Morogoro–Dodoma yenye urefu wa kilomita 260, Barabara ya Handeni–Kiberashi–Chemba–Kwamtoro–Singida (km 384), upanuzi wa Barabara ya Chalinze–Segera–Tanga (km 246), uboreshaji wa Mteremko wa Kitonga (km 27), ujenzi wa Barabara ya Mwendokasi (Expressway) ya Dar es Salaam–Kibaha (km 42), pamoja na Expressway ya Katikati ya Jiji la Dar es Salaam hadi Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) yenye urefu wa kilomita 10.

Leave a Comment