×

Iran Yashutumiwa Kushambulia Meli Mlango wa Hormuz Baada ya Kutoa Onyo

Iran yashutumiwa kufanya shambulio dhidi ya meli ya mizigo iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Singapore katika Mlango wa Hormuz, saa chache baada ya kuonya kuwa meli zitakazokiuka maelekezo yake zinaweza kuchukuliwa hatua.

Kwa mujibu wa maafisa wa Marekani, meli hiyo ilipigwa na ndege isiyo na rubani (drone), na kusababisha uharibifu katika daraja la kuiongozea bila majeruhi. Shirika la Uingereza la UKMTO pia lilithibitisha tukio hilo likisema meli ilishambuliwa karibu na pwani ya Oman.

Kabla ya shambulio hilo, Iran kupitia Walinzi wa Mapinduzi (IRGC) ilitangaza kuwa meli zinapaswa kutumia njia zilizoidhinishwa na Tehran pekee.

Mlango wa Hormuz ni njia muhimu inayopitisha takribani asilimia 20 ya mafuta yanayosafirishwa duniani, hivyo tukio hilo limeongeza hofu ya kuvurugika kwa biashara ya kimataifa na kupanda kwa bei za mafuta. Iran hadi sasa haijatoa tamko rasmi kuhusu madai hayo.

Leave a Comment