×

Timu Zilizofuzu Kuingia Hatua ya 32 Bora Kombe la Dunia Mpaka Sasa

Baada ya mechi za Kundi G kukamilika asubuhi ya leo, huku makundi A hadi I yakihitimisha ratiba zao, jumla ya timu 28 zimejihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya 32 Bora ya Kombe la Dunia 2026.

Hadi sasa, zimebaki nafasi nne pekee kukamilisha orodha ya timu 32 zitakazoshiriki hatua ya mtoano, huku mechi za mwisho za makundi J, K na L zikisubiriwa ili kuamua timu zitakazoungana na zile ambazo tayari zimefuzu.

Kwa upande wa Afrika, timu saba kati ya 10 zilizoshiriki zimefanikiwa kutinga hatua ya 32 Bora. Timu hizo ni Afrika Kusini, Ivory Coast, Cape Verde, Misri, Morocco, Ghana na Senegal.

Kwa upande mwingine, Tunisia imeaga rasmi mashindano hayo baada ya kushindwa kufuzu hatua ya mtoano, huku Algeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) zikisubiri mechi zao za mwisho za makundi ili kujua hatima yao katika mbio za kutinga hatua ya 32 Bora.

Group A: Mexico, South Africa
Group B: Switzerland, Canada, Bosnia & Herzegovina
Group C: Brazil, Morocco
Group D: USA, Australia, Paraguay
Group E: Germany, Côte d’Ivoire, Ecuador
Group F: Netherlands, Japan, Sweden
Group G: Belgium, Egypt
Group H: Spain, Cabo Verde
Group I: France, Norway, Senegal
Group J: Argentina
Group K: Colombia, Portugal
Group L: England, Ghana

Leave a Comment