×

VIDEO: Marehemu Kamanda Abwao Alivyozikwa Kijeshi Kijijini Kwao

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Marehemu Richard Abwao amezikwa katika mazishi yaliyofanyika jana, June 27, 2026 kijijini kwao, Shirati, Rorya mkoani Mara.

Kamanda Abwao alifikwa na mauti wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili National Hospital (MNH) jijini Dar es Salaam.

Kifo cha Abwao kimewagusa watu wengi kutoka nyanja mbalimbali, kuanzia maafisa na wanajeshi wa Jeshi la Polisi, viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi wa kawaida, wengi wakikielezea kama pigo kubwa kutokana na mchango mkubwa aliokuwa nao kwa jeshi na jamii kwa jumla.

Leave a Comment