Druski, Olandria, Doechii Waongoza Listi ya Waliovalia Vizuri BET 2026
Global Publishers June 29, 2026 370 views 0 Comments
SHARE THIS:
Mchekeshaji (comedian), Druski na mtu maarufu wa mitandaoni kutoka Marekani video zake za ucheshi kwenye Instagram, TikTok na YouTube.
LOS ANGELES, Marekani – Zulia jekundu la BET Awards 2026 limekuwa kivutio kikubwa baada ya mastaa mbalimbali wa muziki, filamu na burudani kuonyesha mitindo ya kipekee katika ukumbi wa Peacock Theater jijini Los Angeles.
Miongoni mwa walioiba macho ya kamera ni Druski, ambaye alivalia suti ya kifahari ya rangi ya burgundy, akithibitisha hadhi yake kama mwenyeji wa usiku huo mkubwa wa burudani.
Nyota wa mitindo Olandria Carthen alivutia kwa gauni la njano la shingo wazi lenye mpasuko wa upande, huku akipongezwa kwa muonekano wake wa kipekee ulioteka kamera nyingi.
Mwanamitindo na mtu wa mitandao (social media personality), Olandria Carthen
Msanii Doechii pia alikuwa miongoni mwa waliovutia zaidi, akiwa amevalia gauni la crochet la kahawia, akithibitisha nafasi yake si tu katika muziki bali pia katika mitindo.
Wakati huo huo, mastaa kama Teyana Taylor, Tems, Kehlani na Chlöe Bailey walionekana wakongwe wa mitindo, kila mmoja akionyesha ubunifu wa hali ya juu kwenye mavazi yao.
BET Awards 2026 zimeendelea kuthibitisha kuwa si tu tuzo za muziki, bali pia jukwaa la mitindo ya kiwango cha juu duniani, ambapo mastaa hutumia nafasi hiyo kuonyesha ubunifu wao mbele ya macho ya dunia.
Rapa wa kike kutoka Marekani, Latto.Rapa, mwigizaji na mjasiriamali kutoka Marekani anayejulikana kama mmoja wa waanzilishi wa “Trap Music,” aina ya hip hop iliyotokea Atlanta, T.I.Loren Lorosa mwandishi wa habari za burudani na mtangazaji kutoka Marekani anayejulikana sana kwa kuripoti taarifa za mastaa na tasnia ya muziki, filamu na televisheni.Kehlani mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Marekani anayejulikana kwa muziki wa R&B wenye hisia kali na sauti ya kipekee.The-Dream mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na producer wa muziki kutoka Marekani. Anajulikana sana kwa kuchangia kuandika na kutengeneza nyimbo kubwa za R&B na pop.Trevor Jackson mwigizaji, mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Marekani. Alianza kujulikana akiwa mdogo kupitia majukumu ya uigizaji kwenye televisheni na filamu, kabla ya kuimarisha umaarufu wake kupitia kazi kubwa kama mfululizo wa TV “Black-ish” na “Grown-ish”, ambamo aliigiza mhusika Aaron.JaNa Craig mtu maarufu wa televisheni za reality (reality TV star) kutoka Marekani. Alijulikana zaidi kupitia ushiriki wake kwenye kipindi cha Love Island USA.Rapa wa kike, Flo Milli anayejulikana kwa mtindo wake wa hip hop na ucheshi.Leon Thomas ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na producer kutoka Marekani.Rapa, Mwimbaji, Mwigizaji na Mtangazaji, Queen Latifah.Muni Long ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Marekani anayejulikana kwa R&B ya kisasa yenye hisia na sauti laini.