×

Rais Samia Awaapisha Makatibu Wakuu Wapya, Atoa Mwelekeo wa Utumishi (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Grace Elias Magembe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 01 Julai, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Jumatano, Julai 1, 2026, amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni katika hafla iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, akiwemo Spika wa Bunge, Mussa Zungu.

Miongoni mwa viongozi walioapishwa ni Dk. Grace Magembe, aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya. Kabla ya uteuzi huo, Dk. Magembe alikuwa akihudumu kama Mganga Mkuu wa Serikali.

Pia, Charles Kadonya aliapishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki.

Aidha, Nolasco Kipanda aliapishwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma. Kabla ya uteuzi huo, alikuwa Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Taasisi katika Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Uapisho huo unafuatia uteuzi uliofanywa hivi karibuni na Rais Samia ikiwa ni sehemu ya kuimarisha utendaji na ufanisi katika taasisi mbalimbali za Serikali.

Rais Samia akimuapisha Ndugu Charles Ngeleja Kandonya kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki.
Rais Samia akimuapisha Ndugu Nolasco Jacob Kipanda kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Elias Magembe akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Ndugu Charles Ngeleja Kandonya pamoja na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Ndugu Nolasco Jacob, wakiapa Kiapo cha Maadili, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 01 Julai, 2026.

 

Leave a Comment