×

Pacome Atembelewa Hospitalini na Uongozi wa JKT Tanzania

Uongozi wa Klabu ya JKT Tanzania pamoja na mchezaji Hassan Wahabi wamemtembelea kiungo wa Yanga SC, Pacome Zouzoua leo kwenye hospitali ya Aga Khan, ambaye anaendelea na matibabu hoospitalini hapo baada ya kupata jeraha katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kati ya JKT Tanzania na Yanga SC, uliochezwa Juni 30, 2025, kwenye Uwanja wa Major General Isamuhyo.

Pacome alipata jeraha hilo baada ya kugongana na Hassan Wahabi walipokuwa wakiwania mpira, hali iliyomlazimu kuondolewa uwanjani na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Katika ziara hiyo, viongozi wa JKT Tanzania pamoja na Hassan Wahabi walimjulia hali nyota huyo wa Yanga na kumtakia nafuu ya haraka ili arejee uwanjani kuendelea na majukumu yake.

Kwa upande wake, Yanga SC imepongeza na kuushukuru uongozi wa JKT Tanzania kwa kitendo hicho, ikieleza kuwa ni ishara ya uungwana, mshikamano na ubinadamu inayodhihirisha maadili mema ya michezo.

Klabu hiyo imesisitiza kuwa vitendo vya aina hiyo vinaimarisha urafiki na heshima kati ya timu zinazoshindana, huku vikionesha kuwa ushindani wa uwanjani hauondoi utu, mshikamano na heshima nje ya uwanja.

Leave a Comment