×

Simba Wavunja Ukame! Wabeba Kombe la FA Baada ya Miaka Minne

SIMBA wamefanikiwa kukata kiu ya mataji ya Kombe la FA Tanzania baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC katika fainali iliyopigwa kwenye dimba la Gombani, Pemba.

Ushindi huo umeiwezesha Simba kutwaa CRDB Bank Federation Cup 2025/26 na kurejea kileleni baada ya kukaa misimu minne bila taji hilo. Mara ya mwisho Mnyama kutwaa kombe hilo ilikuwa msimu wa 2020/21.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkali ulipambwa na bao pekee lililoamua matokeo, likitokana na kujifunga kwa Yahya Zayd dakika ya 62, likiipa Simba ushindi muhimu uliowafanya wainyanyue tena kombe hilo kwa mara ya nne tangu kurejea kwa mashindano hayo msimu wa 2015/16.

Azam FC walijitahidi kusaka kusawazisha lakini uimara wa safu ya ulinzi ya Simba uliwazuia na kuhakikisha matokeo yanabaki 1-0 hadi kipenga cha mwisho.

Kwa ushindi huo, Simba SC wanaandika ukurasa mpya wa mafanikio huku mashabiki wao wakisherehekea kurejea kwa taji la FA Cup baada ya miaka ya kusubiri.

Leave a Comment