×

RC Chalamila Atembelea Banda la Yas Sabasaba, Apongeza Suluhisho za Kidijitali kwa Watanzania

Dar es Salaam, Julai 7, 2026 – Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametembelea banda la Yas katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), ambapo alipata fursa ya kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo kwa wananchi.

Mara baada ya kuwasili katika banda hilo, RC Chalamila alipokea maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Yas, Pierre Canton Bacara, kuhusu huduma na suluhisho mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo kwa lengo la kuboresha maisha ya Watanzania kupitia teknolojia na ubunifu.

Miongoni mwa huduma zinazotolewa katika banda hilo ni uchunguzi wa macho bila malipo, mpango wa kumiliki simu janja na rauta za 5G kwa mfumo wa mkopo, huduma za intaneti majumbani na kwa wafanyabiashara kupitia Yas Fiber, pamoja na suluhisho za kidijitali kwa wafanyabiashara na taasisi kupitia Yas Business.

Aidha, wageni wanaotembelea banda hilo wanapata fursa ya kufahamu huduma mbalimbali za kifedha zinazotolewa kupitia Mixx, ambazo zinalenga kurahisisha miamala na kuwawezesha Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali.

Banda la Yas limeendelea kuvutia maelfu ya wageni wanaotembelea Maonesho ya Sabasaba kutokana na ubunifu wa huduma zake na suluhisho zinazokidhi mahitaji ya watu binafsi, wafanyabiashara na taasisi.

Leave a Comment