×

Trump Adai Iran Inataka Kufanya Makubaliano Haraka Sana

Rais wa Marekani, Donald Trump, amedai kuwa Iran imewasiliana naye ikitaka kufikia makubaliano mapya, ikiwa ni mabadiliko makubwa ikilinganishwa na msimamo wake wa awali kuhusu mazungumzo kati ya pande hizo mbili.

Akizungumza akiwa ndani ya ndege ya rais wa Marekani, Air Force One, mara baada ya kutua Maryland akitokea Ankara, Uturuki, alikohudhuria mkutano wa NATO, Trump alisema Iran ilimpigia simu muda mfupi uliopita na kuonyesha nia kubwa ya kufikia makubaliano.

“Walinipigia simu muda mfupi uliopita. Wanataka kufanya makubaliano sana,” alisema Trump.

Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Trump kueleza kuwa usitishaji wa mapigano ulikuwa umefikia mwisho na kwamba mazungumzo na Iran yalikuwa ni kupoteza muda.

Hata hivyo, hadi sasa serikali ya Iran haijatoa tamko lolote la kuthibitisha hadharani madai hayo ya Trump, jambo linaloacha hali ya sintofahamu kuhusu mustakabali wa uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Leave a Comment