
Dar es Salaam, Tanzania, 9 Julai 2026: SportPesa Tanzania leo imemtangaza mshindi mpya wa Mid-Week Jackpot, Latifah Hamisi Mdoka ambaye ni mjasiriamali mwenye umri wa miaka 28 anayeishi Vikindu, Dar es Salaam, aliyejishindia Tsh 268,671,530 kupitia Mid-Week Jackpot ya SportPesa.
Latifah, ambaye ni mzaliwa wa Mchinga mkoani Lindi, anakuwa mshindi wa tano mkubwa wa jackpot mwaka 2026 na mwanamke wa tatu kujishindia jackpot ya mamilioni kupitia SportPesa Tanzania mwaka huu. Alijiunga na SportPesa mwezi Juni 2019 na tangu wakati huo amekuwa mteja hai akishiriki mara kwa mara kwenye Mid-Week Jackpot na Supa Jackpot. Ingawa aliwahi kujishindia bonasi ndogo hapo awali, huu ndio ushindi mkubwa zaidi aliowahi kuupata tangu aanze kushiriki jackpot za SportPesa.
Akizungumzia ushindi wake, Latifah alisema bado haamini kilichotokea na kwamba ndoto aliyokuwa nayo kwa miaka mingi sasa imetimia.
“Nilipopigiwa simu na kuambiwa nimeshinda, kwa kweli sikutegemea kabisa. Nilidhani ni utani. Nimekuwa nikicheza jackpot kwa matumaini kuwa siku moja na mimi ningekuwa mshindi, na leo ndoto hiyo imetimia. Namshukuru Mungu na SportPesa kwa ushindi huu ambao naamini utabadilisha maisha yangu na ya familia yangu,” alisema Latifah.
Mkuu wa Idara ya Masoko wa SportPesa Tanzania, Tracy Humplick, alisema ushindi wa Latifah ni miongoni mwa simulizi nyingi za Watanzania ambao wameendelea kunufaika kupitia jackpot za SportPesa.
“Kinachofurahisha zaidi kuhusu ushindi wa Latifah ni kwamba amekuwa nasi kwa zaidi ya miaka saba. Ameendelea kushiriki kwa uvumilivu na leo ameona matokeo yake. Huu ni uthibitisho kuwa kila anayeshiriki ana nafasi ya kushinda, na tunafurahi kuona ushindi huu ukibadilisha maisha yake,” alisema Tracy.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa Tanzania, Mhe. Tarimba Abbas, alisema kampuni itaendelea kuwapa Watanzania fursa ya kujishindia zawadi kubwa kupitia bidhaa zake mbalimbali.
“Tangu SportPesa ilipoanza shughuli zake nchini Tanzania, tumewatunuku washindi wakubwa 29 wa jackpot wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 8.8. Ushindi wa Latifah unaongeza idadi ya wanawake wanaoendelea kushinda jackpot zetu mwaka huu na unaonesha wazi kuwa washindi wetu wanatoka katika mikoa, taaluma na mazingira mbalimbali nchini. Hii ndiyo dhamira yetu ya kuendelea kuwapa Watanzania nafasi ya kubadilisha maisha yao kupitia jackpot za SportPesa,” alisema Mhe. Tarimba Abbas.
Ushindi wa Latifah unaendelea kuonesha kuwa jackpot za SportPesa zinabadilisha maisha ya Watanzania kutoka maeneo na makundi mbalimbali nchini.