×

Kaze Afunguka Kuhusu Pointi za Simba SC

BIG bosi wa benchi la ufundi la Yanga, Mrundi Cedric Kaze amefunguka kwamba kwake mechi yao na Simba siyo muhimu sana na badala yake anapiga hesabu kwenye mechi nyingine za ligi.

Kocha huyo ameongeza kwamba kwake kila mechi itakuwa fainali kwa kutaka kila pointi ili kukifanya kikosi hicho kifanye vizuri katika ligi kuu.

Kaze aliyesaini mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha Yanga kwa mara ya kwanza ataiongoza klabu hiyo kwenye Dabi ya Kariakoo mbele ya Simba, Novemba 7, katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Kaze amesema kwamba kwake hawezi kuiwaza mechi hiyo na Simba pekee kwani mipango yake ni kuona anashinda mechi zote za ligi ambapo watapambana kama fainali.

“Hatuwezi kuwaza mechi na Simba tu, tunatakiwa kucheza na kushinda mechi nyingine za ligi, tukicheza na Simba pointi ni zilezile.“Tunatakiwa kucheza mechi hizo kama fainali kwa sababu ya kusaka pointi ambazo zitatufanya tukae kwenye eneo zuri la msima.

Stori: Said ally,Dar es Salaam

https://globalpublishers.co.tz/ligi-ya-mabingwa-kuendelea-leo-usiku-ajax-vs-liverpool/

Leave a Comment