
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Zuchu, ametangaza kuwa uhusiano wake wa ndoa na Diamond Platnumz umefikia tamati.
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Zuchu amesema wameamua kuhitimisha ndoa yao kwa makubaliano ya pande zote.
Ameeleza kuwa licha ya kuachana kama wanandoa, wataendelea kushirikiana katika masuala ya kazi na muziki.

Tangazo hilo limezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki, huku wengi wakieleza mshangao wao kutokana na historia ya wawili hao kuwahi kutangaza kuachana na baadaye kurudiana mara kadhaa.
Wakati baadhi ya mashabiki wakituma salamu za kuwapa moyo, wengine wameendelea kutoa maoni wakidai kuwa si mara ya kwanza kwa wawili hao kutoa taarifa za aina hiyo, wakiamini huenda hali ikabadilika tena siku zijazo. Hata hivyo, hadi sasa Zuchu amesisitiza kuwa uamuzi huo umefikiwa kwa makubaliano ya pande zote.

