
STAA wa filamu za Bongo, Irene Uwoya, amefunguka kupitia ukurasa wake wa Insta kuhusu tabia yake katika kushughulika na watu, akisema yeye ni mtu anayependa amani na hana kawaida ya kuwa na migogoro na mtu yeyote.
Irene amesema kuwa mtu akijikuta ana tatizo naye, basi huenda amelifuatilia kwa muda na kutumia juhudi kubwa kulifikia, kwa kuwa yeye si mtu wa kutafuta ugomvi.
“Mimi sina shida na mtu, nina upendo sanaaa… Ila ukiona mtu ana shida na mimi ujue ametumia nguvu sana na muda wa kutosha kuitafuta hiyo shida,” alisema Irene Uwoya.
