×

Rais Samia Afanya Mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Accra nchini Ghana, tarehe 21 Julai, 2026, kwa ajili ya kushiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu Afya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alivyowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Accra nchini Ghana kwa ajili ya kushiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu Afya, unaofanyika Julai 21, 2026.

Mara baada ya kuwasili, Rais Samia alisalimiana na viongozi mbalimbali waliompokea uwanjani, kabla ya kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana, Samuel Okudzeto Ablakwa.

Mkutano huo unawakutanisha viongozi wa nchi za Afrika kujadili masuala muhimu yanayohusu sekta ya afya, ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya huduma za afya, ushirikiano wa kikanda na maandalizi ya kukabiliana na changamoto za kiafya barani Afrika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana  Samuel Okudzeto Ablakwa baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Accra nchini Ghana, tarehe 21 Julai, 2026 kwa ajili ya kushiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu Afya.

Leave a Comment