×

LeBron James Atikisa NBA, Philadelphia 76ers Wathibitisha Kusajili

Philadelphia 76ers wamethibitisha kumsajili nyota wa NBA, LeBron James, ambaye amesema huu utakuwa mkataba wake wa mwisho katika ligi hiyo.

James mwenye umri wa miaka 41 ameondoka Los Angeles Lakers baada ya kuitumikia kwa misimu minane, na sasa ataungana na kikosi chenye wachezaji kama Joel Embiid, Tyrese Maxey, Jaylen Brown na VJ Edgecombe.

Akizungumza baada ya kutangaza uamuzi huo, James alisema anaamini anaweza kusaidia Philadelphia 76ers kutwaa ubingwa wa NBA na anafurahia kuanza safari mpya na mashabiki wa Philadelphia.

Kwa mujibu wa ESPN, James amesaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya dola milioni 8, ukiwa na chaguo la mchezaji (player option) kwa mwaka wa pili.

Kabla ya kuchagua Philadelphia 76ers, James alihusishwa na vilabu kadhaa ikiwemo Cleveland Cavaliers, Golden State Warriors, Minnesota Timberwolves na Miami Heat.

LeBron James ndiye mfungaji bora wa muda wote katika historia ya NBA, ameshinda ubingwa wa NBA mara nne na kutwaa tuzo ya MVP wa Fainali mara nne, huku pia akichaguliwa kwenye kikosi cha NBA All-Star kwa misimu 22 mfululizo.

Leave a Comment