Meridianbet imechukua nafasi kubwa kwenye jukwaa la UFC baada ya kuwa mdhamini wa UFC Fight Night, tukio lililofanyika Agosti 1, 2026 kule Belgrade Arena, Serbia. Udhamini huo uliifanya Meridianbet kuwa sehemu ya usiku mkubwa wa MMA, huku mashabiki wakishuhudia burudani ya kiwango cha juu na chapa hiyo ikiendelea kuimarisha uwepo wake katika ulimwengu wa michezo ya kimataifa.
Na kama vile jina la Meridianbet lilivyokuwa kwenye tukio, pambano kuu lenyewe lilitoa burudani ya kutosha. Uroš Medić, akiwa mbele ya mashabiki wake wa nyumbani, alimshangaza Daniel Rodriguez kwa kumaliza pambano ndani ya sekunde 30 tu za raundi ya kwanza. Medić alitumia mbinu sahihi kumuangusha Rodriguez na kumlazimisha mwamuzi kusimamisha pambano mapema.
Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Takwimu zinaonyesha wazi ukubwa wa mashambulizi ya Medić. Katika sekunde hizo 30, alifanikiwa kuunganisha mashambulizi 11 kati ya 14, sawa na asilimia 78 ya usahihi, wakati Rodriguez aliunganisha shambulio moja pekee kati ya matatu. Kwa mashabiki waliokuwa wakifuatilia tukio hilo, ilikuwa ni burudani ya haraka, kali na isiyotarajiwa kumalizika mapema kiasi hicho.
Usiku huo ulikuwa na sura nyingine ya Meridian pia, baada ya Michael “PQD” Oliveira, anayefadhiliwa na Meridianbet Brazil, kufanya ushiriki wake wa kwanza ndani ya UFC na kupata ushindi wa knockout katika raundi ya kwanza. Hivyo, Meridian iliunganishwa moja kwa moja na matukio mawili makubwa ya usiku huo, ushindi wa Medić katika pambano kuu na mwanzo wa Oliveira kwenye jukwaa la UFC.
Kwa Meridianbet, udhamini wa UFC Fight Night ulikuwa ujumbe wa nguvu kuhusu nafasi ya chapa katika michezo ya kimataifa. Kutoka Belgrade hadi kwa mashabiki wa MMA duniani, Meridianbet ilipata jukwaa la kuonyesha uwezo wake wa kuungana na matukio makubwa, yenye ushindani na yenye hadhira kubwa.