
Klabu ya Yanga SC, maarufu kama Wananchi, imemtambulisha mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Selemani Mwalimu ‘Gomez’, kuwa mchezaji wao mpya kuelekea msimu wa 2026/27.
Hatua hiyo imekuja licha ya Simba SC awali kuthibitisha kuwa imefikia makubaliano na Wydad Casablanca ya Morocco kuhusu usajili wa mshambuliaji huyo na kudai kuwa ni mali yao.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC alithibitisha suala hilo Agosti 8, 2026, wakati wa tamasha la Simba Day 2026, akibainisha kuwa Gomez alikuwa angani akirejea Tanzania kutoka Morocco.