
Watu 132 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 570 wakiripotiwa kujeruhiwa kutokana na tetemeko la ardhi lilioikumba Colombia Agosti 10.
Tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa wa 7.4 na lilipiga maeneo ya magharibi mwa Colombia, na kusabibisha kuanguka kwa majengo, uharibifu wa miundombinu na kuwaacha baadhi ya watu wakiwa wamenaswa chini ya vifusi.
Vikosi vya uokoaji vinaendelea kutafuta watu wanaodhaniwa kuwa wamekwama kwenye majengo yaliyoporomoka, huku wanajeshi, polisi na wafanyakazi wa uokoaji wakipelekwa katika maeneo yaliyoathirika.
Mji wa Cali ni miongoni mwa maeneo yaliyoripotiwa kuathirika zaidi, huku hospitali na majengo mengine yakikumbwa na uharibifu.

Serikali ya Colombia imetangaza hali ya dharura na kuimarisha shughuli za uokoaji na utoaji wa msaada kwa watu waliopoteza makazi kutokana na maafa hayo.
Mamalaka ya Anga nchini humo imesitisha safari ndege kwa baadhi ya kutokana miundombinu ya viwanja kuharibika kutokana na tetemeko hilo.
Wataalamu wa tetemeko wameonya kuhusu uwezekano wa mitikisiko mingine, huku juhudi za uokoaji na tathmini ya madhara zikiendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Tetemeko hilo limekuwa moja ya majanga makubwa zaidi ya asili kuikumba Colombia katika kipindi cha hivi karibuni, huku idadi ya vifo ikitarajiwa kubadilika kadiri shughuli za uokoaji zinavyoendelea.
Mwaka 1999 Colombia ilikumbwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa magnitudi 6.2 lilosababisha vifo vya watu 1000.
Na Munira Maridadi.