×

Penzi la Kiredio na Vee Dollarz Lavunjika Tena, Madai Mazito Yaibuka

Mtangazaji na muandaaji wa maudhui, Vicent Njau maarufu kama Kiredio akiwa na mpenzi wake Vee Dollarz.

Mtangazaji na muandaaji wa maudhui, Vicent Njau maarufu kama Kiredio, inasemekana kuwa amepigwa tukio na watu wenye pesa baada ya kumchukua mpenzi wake Vee Dollarz, hali iliyopelekea penzi hilo kuvunjika kwa mara ya pili.

Mashabiki mbalimbali mitandaoni wamekuwa wakisema kuwa walimuonya Kiredio kutomuingiza mpenzi wake huyo kwenye maisha ya mitandao, jambo ambalo kwa mujibu wao limepelekea kuwa na macho mengi kwenye uhusiano wao.

Wameendelea kusema kuwa Vee Dollarz ni msichana anayependa maisha ya gharama kubwa, huku wakidai kuwa kipato cha Kiredio bado ni kidogo kumtunza mrembo huyo.

Mashabiki hao wameweka wazi kuwa kwenye mitandao wanaume wengi wanatamani kuwa na Vee Dollarz, huku baadhi yao wakidaiwa kutokuwa na maneno mengi bali kumuomba namba ya akaunti yake ya benki na kumuingizia zaidi ya Sh milioni 20 kwenye akaunti yake.

Kwa upande wa Kiredio, kupitia mitandao ya kijamii, alisema kuwa watu walio kwenye ndoa na wenye pesa wamekuwa wakichukua wapenzi wa watu wengine na wao kupotezea, lakini ikitokea wao wamewachukulia wake zao, huwachukulia hatua.

Maneno hayo yanadaiwa kusemwa na Kiredio kupitia Instagram Status yake hivi karibuni.

Mashabiki hao wamemaliza kwa kutoa ushauri kwa Kiredio, wakisema iwapo yeye na Vee Dollarz watarudiana, Vee anatakiwa kuondoka kwenye mitandao ili kuepusha macho na usumbufu wa watu kwenye uhusiano wao.

Leave a Comment