
Petro de Luanda imetangaza rasmi kumsajili tena mshambuliaji wa Kimataifa wa Angola, Laurindo Dilson Maria Aurélio ‘Depú’, kutoka Yanga, kuelekea msimu wa 2026/27.
Uhamisho huo umegharimu USD 500,000, sawa na takribani TSh bilioni 1.3.
Kupitia taarifa yao, Petro de Luanda wamemkaribisha Depú kwa kusema:
“Ameirejea katika sehemu ambayo anakuwa mwenye furaha. Karibu tena, Depú!”