×

Yanga Yakataa Ofa ya Tsh bilioni 1.8 kwa Allan Okello

Yanga wanadaiwa kukataa ofa ya dola 700,000, sawa na takribani Tsh bilioni 1.8, kutoka FAR Rabat ya Morocco kwa ajili ya kumsajili kiungo mshambuliaji wake, Allan Okello.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, FAR Rabat jana iliwasilisha ofa hiyo kwa Yanga ikiwa na lengo la kumnasa nyota huyo wa Uganda, lakini klabu hiyo ya Jangwani imekataa kiasi hicho.

Yanga imeeleza kuwa ipo tayari kumuuza Okello iwapo FAR Rabat itafikia dau la dola milioni 1.5, ambalo ni sawa na takribani Tsh bilioni 3.9.

Uamuzi huo unaonyesha namna Yanga inavyomthamini Okello, huku klabu hiyo ikiamini kuwa thamani yake sokoni inaweza kufikia kiwango kinacholingana na fedha iliyowahi kulipwa kwa nyota kama Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Wakati FAR Rabat ikisaka huduma ya Okello, taarifa zinaeleza kuwa Wydad AC nayo imeanza kufuatilia uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo, hali inayoweza kuongeza ushindani katika mbio za kumpata.

Leave a Comment