
Mfanyabiashara maarufu nchini, Jennifer Bilikwija, anayefahamika kwa jina la Niffer, amezua gumzo baada ya kueleza mtazamo wake kuhusu kuwa na urafiki wa karibu na wanawake wenzake.
Niffer kupitia kauli yake amesema licha ya kuwapenda na kuwathamini wanawake wenzake, suala la kuwa na urafiki wa karibu si jambo analoweza kulifanya.
“Yan nawapenda wanawake wenzangu ila kuwa na urafiki wa karibu nao siwezi kabisaaaa.” 😆🙌🙌🥹😹”
Kauli hiyo imepokea hisia tofauti kutoka kwa mashabiki na wafuatiliaji wake mitandaoni, huku baadhi wakihusisha kauli hiyo na uzoefu wa urafiki wa karibu na wanawake.
Niffer hakueleza kwa undani sababu iliyomfanya awe na mtazamo huo, lakini namna alivyoweka emoji za kucheka na kushangaa imeifanya kauli hiyo ionekane zaidi kama mtazamo wake binafsi wenye utani.
Kauli hiyo imeibua mjadala miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kuhusu urafiki wa karibu kati ya wanawake na changamoto zinazoweza kujitokeza katika mahusiano hayo.