×

Bela Ampiga Benchi Mzungu

 

Bella (kulia) akiwa na Baby Madaha Global Tv

Na HAMIDA HASSAN| IJUMAA WIKIENDA| HABARI

DAR ES SALAAM: Ujio wa mfanyabiashara wa Kibongo mwenye maskani yake nchini Uganda, Jackson Akim Pemba ‘Jack Pemba’ ndani ya Jiji la Dar umemfanya msanii wa muziki wa Kundi la Scorpion Girls, Isabela Mpanda ‘Bela’kumpiga benchi mpenzi wake (Mzungu) anayefahamika kwa jina la Criss ili kutanua na jamaa huyo. 

Jack Pemba

Mara baada ya kutua Ijumaa iliyopita, wawili hao walionekana Klabu ya Element iliyopo Masaki, Dar wakijiachia na Bela alipohojiwa kuhusiana na kumbwaga Mzungu alisema kuwa, kwa sasa amemuweka pembeni kwa muda hadi Jack Pemba atakapoondoka.

“Kwa sasa Mzungu wangu yuko pembeni najiachia na Jack kwanza, hayo mambo mengine tutajua baadaye, kwani wewe unamuona Mzungu hapa au unamuona Mwafrika mwenzangu?” Alihoji Bela huku pembeni Jack Pemba akionesha tabasamu la kufurahia maneno ya mrembo huyo.