
Mshambuliaji wa Atlético Madrid, Julián Álvarez, ameamua kuendelea kusalia katika klabu hiyo licha ya kuwepo kwa taarifa za kuhusishwa na uhamisho kuelekea klabu mbalimbali, ikiwemo Arsenal.
Álvarez, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Argentina, alikuwa miongoni mwa mastaa waliokuwa wakitajwa katika siku za mwisho za dirisha la usajili, huku Arsenal ikitajwa kuwa moja ya klabu zilizokuwa na nia ya kupata huduma yake.
Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa Álvarez hakuwa na mpango wa kufanya uhamisho wa dakika za mwisho na badala yake aliendelea na programu yake ya mazoezi akiwa na Atlético Madrid.
Mshambuliaji huyo pia ameripotiwa kufunga milango kwa Arsenal pamoja na klabu nyingine zilizokuwa zikimfuatilia katika dirisha hili la usajili.
Inadaiwa kuwa Barcelona ndiyo klabu pekee ambayo Álvarez alikuwa tayari kujiunga nayo endapo angeamua kuondoka Atlético Madrid.
Hata hivyo, Atlético Madrid ilikuwa imeweka msimamo kwamba haikuwa tayari kufanya biashara na Barcelona kuhusu nyota huyo, jambo lililofanya uwezekano wa uhamisho huo kuwa mgumu.
Kutokana na hali hiyo, Álvarez sasa anatarajiwa kuendelea na maisha yake Atlético Madrid na kuwa sehemu muhimu ya mipango ya kocha Diego Simeone kwa msimu huu.
Uamuzi huo unamaanisha kuwa Arsenal imelazimika kukosa huduma ya mmoja wa washambuliaji waliokuwa kwenye orodha yake ya wachezaji wanaowafuatilia, huku Atlético Madrid ikifanikiwa kumbakisha nyota wake.
Álvarez alijiunga na Atlético Madrid akitokea Manchester City na tangu wakati huo amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu katika safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.
Kwa sasa, macho yanaelekezwa kwenye namna mshambuliaji huyo atakavyore.
Na Didas Didas | GPL