×

TRC Yatangaza Nafasi 24 za Ajira, Waombaji Wapewa Hadi Septemba 10

Dodoma, Agosti 28, 2026 — Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS), kwa niaba ya Tanzania Railways Corporation (TRC), imetangaza nafasi 24 za ajira kwa Watanzania wenye sifa, uwezo na uzoefu unaohitajika.

Nafasi hizo zimetangazwa kupitia tangazo lenye Kumb. Na. JA.9/16/01/53 la tarehe 28 Agosti 2026.

Nafasi zilizotangazwa

  1. Instructor II (Civil Engineer) — Nafasi 1
  2. Instructor II (Mechanical Engineer) — Nafasi 1
  3. Artisan II (Auto Electric) — Nafasi 5
  4. Technician II (Automobile) — Nafasi 4
  5. Technician II (Hydraulic Machineries) — Nafasi 2
  6. Engineer II (Signal & Telecommunication) — Nafasi 1
  7. Locomotive Driver II — Nafasi 10

Sifa za jumla kwa baadhi ya nafasi

Instructor II (Civil Engineer):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Uhandisi wa Ujenzi (Civil Engineering) au taaluma inayolingana nayo, yenye kiwango cha NTA Level 8 au sawa, kutoka taasisi inayotambuliwa. Anatakiwa kuwa na GPA isiyopungua 3.5, pamoja na kuwa anastahili kusajiliwa kama mwalimu wa ufundi na kusajiliwa na bodi husika kama Graduate Engineer/Professional.

Instructor II (Mechanical Engineer):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Mechanical Engineering au inayolingana nayo, yenye kiwango cha NTA Level 8 au sawa, kutoka taasisi inayotambuliwa, akiwa na GPA isiyopungua 3.5. Pia anatakiwa kuwa anastahili kusajiliwa kama mwalimu wa ufundi na kusajiliwa na bodi husika kama Graduate Engineer/Professional.

Artisan II (Auto Electric):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne pamoja na CBET Level II/III, Trade Test Grade I/II au NVA II/III katika fani ya Auto Electric au sifa inayolingana nayo kutoka taasisi inayotambuliwa.

Technician II (Automobile):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne au Sita pamoja na Diploma/NTA Level 6 katika Automobile Engineering, Automotive Mechanics au sifa nyingine inayohusiana na fani hiyo.

Technician II (Hydraulic Machineries):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne au Sita pamoja na Full Technician Certificate (FTC) au Ordinary Diploma in Mechanical Engineering yenye utaalamu wa Hydraulic Machineries au sifa inayolingana nayo.

Engineer II (Signal & Telecommunication):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Electrical Engineering, Telecommunication Engineering, Electronics Engineering au inayolingana nayo kutoka taasisi inayotambuliwa na awe amesajiliwa na Engineers Registration Board (ERB) kama Graduate Engineer.

Locomotive Driver II:
Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne, Cheti cha Uendeshaji Treni (Locomotive Driving Certificate) cha miaka miwili au Locomotive Shunting Certificate kutoka TIRTEC au taasisi inayotambuliwa, pamoja na leseni ya udereva ya Class F au G.

Masharti muhimu ya maombi

PSRS imesema waombaji wote lazima wawe raia wa Tanzania na kwa ujumla wasizidi umri wa miaka 45.

Waombaji wanatakiwa kuambatanisha nakala zilizothibitishwa za vyeti vyao vya elimu na taaluma, pamoja na transcripts na vyeti vya usajili wa kitaaluma kutoka bodi au mamlaka husika pale inapohitajika.

Aidha, mwombaji anatakiwa kupakia picha ya Passport Size ya hivi karibuni katika mfumo wa maombi.

PSRS imesisitiza kuwa result slips za Form IV na Form VI, testimonials pamoja na partial transcripts hazitakubalika kama nyaraka za maombi.

Waombaji wanapaswa pia kutaja referees watatu wanaotambulika na kutoa mawasiliano yao yanayoaminika.

Kwa waombaji wenye vyeti vya elimu vya nje ya Tanzania, vyeti hivyo vinapaswa kutambuliwa na mamlaka husika, ikiwemo TCU, NECTA au NACTVET, kulingana na aina ya sifa.

Jinsi ya kutuma maombi

Maombi yote yanatakiwa kuwasilishwa mtandaoni kupitia Recruitment Portal ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Waombaji wanaweza kutumia:

portal.ajira.go.tz

Barua ya maombi inapaswa kuandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza, kusainiwa na kuelekezwa kwa:

Secretary,
President’s Office, Public Service Recruitment Secretariat,
P.O. Box 2320,
Mahakama Street, Tambukareli,
Dodoma.

Mwisho wa kutuma maombi

Mwisho wa kutuma maombi ni Septemba 10, 2026.

PSRS imesema maombi yatakayowasilishwa kupitia njia nyingine tofauti na Recruitment Portal hayatazingatiwa.

Aidha, ni waombaji watakaoteuliwa pekee ndio watakaotaarifiwa kuhusu tarehe ya usaili.

Sekretarieti imeonya kuwa mtu atakayewasilisha vyeti vya kughushi au taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kisheria.

Leave a Comment