×

Massanza Apigwa Faini ya Mil 10, Bodi ya Ligi Yatembeza Faini Polisi na Geita Gold

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) leo Septemba 4, 2026 imetangaza adhabu mbalimbali dhidi ya klabu, viongozi na waamuzi kutokana na makosa yaliyotokea katika michezo ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/27.

Katika taarifa iliyotolewa Septemba 4, 2026, TPLB imesema adhabu hizo zimehusisha makosa ya nidhamu, kuchelewa uwanjani, kukiuka taratibu za mechi pamoja na udhibiti wa waandishi wa habari.

SINGIDA BLACK STARS NA POLISI TANZANIA KUPIGWA FAINI

Katika mchezo namba 017 kati ya Singida Black Stars na Simba SC, uliomalizika kwa Simba SC kushinda 2-1, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Singida Black Stars, Hussein Massanza, ametozwa faini ya Sh milioni 10.

Massanza ameadhibiwa kwa kosa la kushutumu na kutoa lugha ya matusi kwa waamuzi wa kati na wa pembeni baada ya mchezo, kinyume na Kanuni za Ligi Kuu kuhusu udhibiti kwa maofisa habari wa klabu.

Kwa upande mwingine, Afisa wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Singida Black Stars, Pablo Almasi, naye amepigwa faini ya Sh milioni 10 kwa kosa la kusambaza machapisho kwenye ukurasa wake wa Instagram yaliyoletea madharau na kumkashifu mwamuzi wa mchezo kati ya Young Africans na Coastal Union, pamoja na kuikebehi teknolojia ya Football Video Support (FVS).

Aidha, Polisi Tanzania imepata faini ya Sh milioni 10 kwa kosa la kumjumisha mchezaji mmoja kwenye orodha ya wachezaji 21 kwa ajili ya mchezo dhidi ya Singida Black Stars, kinyume na taratibu za mashindano.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Singida Black Stars, Hussein Massanza.

NAMUNGO YAADHIBIWA KWA KUCHELEWA UWANJANI

Katika mchezo namba 032 kati ya JKT Tanzania na Namungo FC, uliomalizika kwa JKT Tanzania kushinda 2-1, Namungo FC imepewa Onyo Kali kwa kosa la kuchelewa kuwasili kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kwa ajili ya mchezo uliochezwa Agosti 29, 2026.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Namungo iliwasili uwanjani saa 1:55 usiku, wakati mechi ilipangwa kuanza saa 1:30 usiku, jambo ambalo ni kinyume na kanuni za Ligi Kuu kuhusu taratibu za mechi.

TPLB imewakumbusha timu zote kuzingatia kikamilifu kanuni hiyo.

GEITA GOLD YATOZWA SH MILIONI 10

Katika mchezo namba 033 kati ya Simba SC na Geita Gold, uliomalizika kwa Simba kushinda 2-0, Geita Gold imepewa Onyo Kali kwa kosa la maafisa wake kuchelewa kwa dakika 15 kufika katika kikao cha kitaalamu cha maandalizi na uratibu wa mchezo.

Pia, klabu hiyo imepigwa faini ya Sh milioni 10 kwa kosa la kuwakilishwa na maafisa wawili pekee katika kikao hicho, kinyume na matakwa ya kanuni za Ligi Kuu.

AZAM FC YAONYA, WATU WAWILI WAFUNGIWA

Katika mchezo kati ya Kagera Sugar na Azam FC, uliomalizika kwa Azam FC kushinda 2-0, Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imefuta adhabu ya kadi nyekundu aliyokuwa ameonyeshwa Gibril Sillah, mchezaji wa Azam FC, baada ya kujiridhisha kupitia picha kwamba tukio hilo halikustahili adhabu hiyo.

Hata hivyo, Mwamizi wa akiba wa mchezo huo, Greyson Buchard wa Kagera, amepewa Onyo Kali kwa kosa la kuonesha mapungufu ya kiuchezaji yaliyotokana na kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu.

Aidha, Azam FC imepewa Onyo Kali kwa kosa la kuwakilishwa na Kocha Msaidizi katika Mkutano wa Wanahabari siku moja kabla ya mchezo, kinyume na taratibu za Ligi Kuu.

KOCHA JOHN ZONGWE AFUNGIWA MIEZI 12

Katika taarifa hiyo, TPLB pia imetangaza kufungiwa kwa miezi 12 kwa aliyekuwa Kocha Mkuu wa IAA, John Zongwe.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Zongwe aliwasilisha ombi la kupunguziwa adhabu baada ya kufungiwa kwa kipindi cha miezi 12, akieleza kuwa amejifunza kutokana na adhabu hiyo na kuahidi kuwa balozi mzuri kwa makocha wengine.

Hata hivyo, TPLB imesema Zongwe alifungiwa baada ya kubainika kumchezesha mchezaji ambaye katika mchakato wa usajili wake alitumia jina la Joseph Ombeni, badala ya Bryson Urio, jambo lililokiuka taratibu za usajili wa wachezaji.

Zongwe pia alikuwa tayari ametumikia miezi sita ya adhabu hiyo, huku akizingatiwa katika uamuzi wa kumruhusu kurejea kwenye shughuli za mpira wa miguu.

TPLB imesisitiza kuwa hatua hizo zinalenga kuhakikisha klabu, viongozi, wachezaji na wadau wote wanazingatia kanuni za Ligi Kuu na taratibu za mchezo.

Leave a Comment