×

Kauli za Brenda Rupia Kizimbani zawa Kivutio Kesi Ya Lissu, Akamilisha Ushahidi

Shahidi wa nne wa upande wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, Brenda Rupia, amekamilisha kutoa ushahidi wake leo Septemba 9, 2026.

Rupia, ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, amekuwa akijibu maswali ya mawakili wa Serikali kuhusu hotuba mbalimbali za Lissu, ikiwemo kauli zinazodaiwa kuwa na maneno kama “tutahamasisha uasi”“hakuna reforms, hakuna uchaguzi” na “tutakinukisha.”

Katika dodoso hilo, Wakili wa Serikali, Katuga, alimuuliza Rupia kuhusu video ya Lissu aliyosema aliiona kupitia YouTube ya Jambo TV. Shahidi alithibitisha kuiona video hiyo, akisema Lissu alikuwa amevaa vazi la combat, ingawa hakukumbuka rangi ya vazi hilo wala kama alikuwa amevaa miwani.

Rupia pia alikiri kuwa katika video hiyo kulikuwa na bendera ya Taifa, huku alipoulizwa kuhusu bendera ya CHADEMA akisema hakumbuki na kuomba sehemu hiyo ya ushahidi ifutwe.

Katika sehemu nyingine ya ushahidi, Rupia alikiri kwamba Lissu alitumia neno “uasi”, lakini alieleza kuwa kwa uelewa wake kauli hiyo ililenga kupinga sheria kandamizi.

Brenda Rupia, ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chadema.

Alipoulizwa kuhusu kauli ya CHADEMA ya “No Reforms, No Election”, Rupia alisema ilikuwa ni msimamo wa chama uliomaanisha kuwa bila mabadiliko hakutakuwa na uchaguzi, lakini akasisitiza kuwa chama hakikusema kingezuia uchaguzi.

Wakili Katuga pia alimuuliza shahidi kama Lissu alielekeza njia za kuvuruga uchaguzi au “kukinu­kisha”, ambapo Rupia alijibu kuwa alielekeza.

Kwa upande wake, Wakili Job alimuuliza Rupia kuhusu majukumu yake kama Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA. Shahidi alieleza kuwa moja ya majukumu yake ni kuratibu mawasiliano ya chama na umma kupitia vyombo vya habari, pamoja na kusimamia utendaji wa watu walio chini ya idara yake.

Rupia pia alieleza kuwa ana elimu ya Accounting na hakusomea uandishi wa habari, lakini akasisitiza kuwa anasimamia idara nzima ya mawasiliano ya chama.

Katika maswali ya Wakili Tawabu Issa Tawabu, Rupia alisisitiza kuwa kwa mtazamo wake Lissu hakufanya kosa, huku akisema mamlaka ya mwisho ya kuamua kama mtu ametenda kosa ni mahakama.

Alipoulizwa maana ya uhaini, Rupia alisema kwa uelewa wake ni kuisaliti nchi au kutaka kupindua serikali. Kuhusu uasi, alitoa tafsiri kuwa ni kitendo cha kikundi cha watu kupinga au kubadili mfumo wa nchi bila kufuata sheria.

Wakili Tawabu pia alimuuliza kuhusu umiliki wa maudhui yaliyotangazwa na Jambo TV. Rupia alisema maudhui hayo ni mali ya chombo husika cha habari na kwamba Lissu si mmiliki wa Jambo TV wala maudhui hayo.

Wakati wa maswali ya Wakili Cuthbert Mbiling’i, Rupia alikiri kuwa yeye ni kiongozi wa CHADEMA na kwamba amekuwa mwanachama wa chama hicho tangu mwaka 2013. Alikubali pia kuwa ushahidi anaoutoa ni wa kumtetea kiongozi wake, lakini akasema yeye ni “shahidi mwenye interest ya haki kutendeka”, si kwa sababu ya kumlinda Lissu bila kujali ukweli.

Rupia pia alithibitisha kuwa Lissu alitamka maneno “uasi” na “tutakinukisha”, lakini akasisitiza kuwa maneno hayo hayakuwa kosa kwa uelewa wake.

Katika maswali ya Wakili Winniwa, shahidi alieleza tafsiri yake ya neno “uasi” kuwa ni kupinga au kukataa kwa nguvu kubwa. Alipoulizwa maana ya “kukinikisha”, alisema linahusiana na kitu kunukia au kunuka vibaya, akitoa mfano wa mtu anayepika pilau na harufu yake kuwafanya wengine watambue kuwa kuna mtu anapika.

Baada ya mawakili wa Serikali kukamilisha maswali yao, Jaji alitangaza kuahirisha mwenendo wa kesi hadi kesho saa 3:00 asubuhi, huku upande wa utetezi ukiendelea na hatua zake katika kesi hiyo.

Shahidi wa tano wa upande wa utetezi anatarajiwa kuendelea na ushahidi katika hatua inayofuata ya kesi hiyo.

Baada ya kukamilika kwa hatua hiyo, majaji waliiahirisha kesi hiyo kwa muda wa saa moja na nusu, hadi saa 8:30 mchana, ambapo shahidi wa tano wa upande wa utetezi anatarajiwa kupanda kizimbani kuanza kutoa ushahidi katika kumtetea Lissu.

  • Katuga: Waambie majaji kama ulifanikiwa kuona video ya mwemyekiti kwenye mtandao wa youtube wa jambo Tv.

    Brenda: Ndio nilifanikiwa kuiona.

    Katuga: Mshtakiwa alikuwa ameonekana amevaa nini?

    Brenda: Nguo za Chama Combat

    Katuga: Alikuwa amevaa combat ya rangi gani?

    Brenda: Sikumbuki.

    Katuga: Alikuwa amevaa miwani?

    Brenda: Sikumbuki

    Katuga: Ni kweli kwamba ndani ya kombat alikuwa amevaa tshirt nyeusi?

    Brenda:Sikumbuki

    Katuga: Kama uliona hiyo video kwenye nyuma kulikuwa na bendera ya taifa na chama.

    Brenda: Ndio ni kweli kulikuwa bendera ya taifa na chadema.

    Katuga: Bendera ya Chadema ina rangi gani?

    Brenda: Blue, nyeupe na nyekundu

    Katuga: Waambie majaji kama unakumbuka mashahidi waliosema wameona hii video na unakumbuka ushahidi wao wakisema walimuona mwenyekiti akiwa amevaa miwani, kombat na nyuma yake kuna bendera ya taifa na chadema.

    Brenda: Sikumbuki

    Katuga: Hawa mashahidi waliambia mahakama walimuona lissu amevaa kombat sasa wewe na hawa mashahidi nani alisema uongo

    Brenda: Sikumbuki.

    Katuga: Unajua vitu vingine ni virahisi kama hawa mashahidi wamesema kwamba alikuwa amevaa kombat na nyuma yake kuna bendera.

    Brenda: Ni ushahidi wangu kwamba mwenyekiti alikuwa amesimama nyuma kuna bendera ya taifa ila kama kuna bendera ya chadema sikumbuki naomba mfute hiyo.

    Katuga: Waambie majaji kama ulisikia akisema majaji ni maccm.

    Brenda: Sikumbuki.

    Katuga: Waambie majaji kama alisema mahakamani hakuendeki.

    Brenda: Sikumbuki

    Katuga: Waambie majaji kama ukisikia watafanyaje watatuua si watanikamata na kunifungulia kesi ya uhaini?

    Brenda: Ndio

    Katuga: Wakati unamsikia mwenyekiti akisema atashtakiwa kwa uhaini hii kesi ilikuwa imefunguliwa?

    Brenda: Hapana

    Katuga: Una mamlaka gani kusema kesi hii ni ya uongo?

    Brenda: Mahakama ndio ina mamlaka kisheria Mimi sina mamlaka

    Katuga: Ulisikia akisema mapolisi wanaingia na kura feki kwenye vibegi mgongoni.

    Brenda:Nilimsikia.

    Katuga: Unajua kama mshtakiwa ana kesi ya kutoa taarifa uongo Kisutu?

    Brenda: Sifahamu

    Katuga: Yaani hufahamu ?

    Brenda: Naomba nikumbushe kama yapo.

    Katuga: Waambie majaji kama mwenyekiti hakutaka hotuba yake ifikie umma.

    Brenda: Sijui kama alitaka au hakutaka.

    Katuga: Waeleze majaji kama unajua mh lissu ana vyombo vyake binafsi vya kutoa taarifa zake.

    Brenda: Sijui kama ana vyombo binafsi.

    Katuga: Waambie majaji wakati mwenyekiti anataka kutoa taarifa yake kwa umma huwa anafanya nini kuufikia umma?

    Brenda: Sijui.

    Katuga:Unajua au hujui kwamba mwenyekiti akitaka taarifa ifike kwa umma anaongea na waandishi wa habari.

    Brenda: Anafanya press conference.

    Katuga: Kwa hiyo ni ushahidi wako kwamba bwana mshtakiwa njia pekee anayotumia kuchapisha taarifa yake kwa wananchi ni kupitia vyombo vya habari.

    Katuga: Neno uasi lazima lielekezwe dhidi ya watu fulani.

    Brenda: Ni dhidi ya mtu watu fulani ni sahihi.

    Katuga: Waambie majaji hili neno tutahamasisha uasi ambalo unasema ulisikia mwenyekiti akilisema ilikua kuhamasisha uasi dhidi ya nani?

    Brenda: Dhidi ya sheria kandamizi.

    Katuga: Sasa waambie majaji ile kuhamasisha uasi dhidi ya sheria ilikuwa ni kuichana hii sheria.

    Brenda: Dhidi ya sheria kandamizi.

    Katuga umezitaja.

    Brenda: Sijataja naomba nizitaje waheshimiwa majaji.

    Katuga: Hivi mabadiliko ya kisiasa yanafanywa na watu au taratibu za kisheria.

    Brenda: Nguvu na mamlaka ni ya watu hivyo watu ndio wanafanya mabadiliko.

    Katuga: Uasi unaenda dhidi ya mfumo na watu wenye mamlaka au dhidi ya sheria kandamizi.

    Katuga: Aliposema tutahamasisha uasi waambie waheshimiwa mtazuia sheria zisifanye uchaguzi au mtazuia watu.

    Brenda: Yalilenga sheria kubadilishwa.

    Katuga: Waambie majaji kwamba sheria ndio zinashiriki kupiga kura.

    Brenda: Hapana.

    Katuga: Unaenda kuzuia watu wasipige kura au sheria.

    Brenda: Sheria.

    Katuga: Nani wanapiga kura?

    Brenda: Watu wanapiga kura.

    Katuga: Unapozuia uchaguzi unamanisha nini unazuia watu au?

    Brenda: Unazuia mchakato mzima.

    Katuga: Unajua au hujui kama chadema inaamini katika demokrasia

    Brenda: Iko kwenye falsafa ya chama.

    Katuga: Unajua Tanzania iko katika mfumo wa vyama vingi?

    Brenda: Ndio.

    Katuga: Waambie majaji kama hii no reforms no election ilikuwa katika msimamo wa chama.

    Brenda: Ndio

    Katuga: Kuna ushahidi hapa mahakamani kwamba no reforms no election ni msimamo uliolenga kuzuia uchaguzi mpaka mabadiliko yafanyike.

    Brenda: Sio kweli ni msimamo wa chama hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi.

    Katuga: Niko sahihi kusema chadema ilimaanisha kama hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi.

    Brenda: ilisema hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi haikusema itazuaia uchaguzi.

    Katuga: Unafahamu uchaguzi upo kwa mujibu wa katiba?

    Brenda: Nafahamu.

    Katuga: Waambie majaji kama unafahamu kubadili katiba ni mchakato.Waambie majaji kwa kuwa wewe unatuambia katiba ni mchakato na uchaguzi uko kwa mujibu wa katiba mlioanza kusema kama hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi na no reforms ilianza 2024.

    Katuga: Iambie mahakama ilipanga vipi kuzuia uchaguzi katika hotuba yake.

    Brenda: Alielekeza.

    Katuga: Alielekeza njia za kuvuruga uchaguzi?

    Brenda: Alielekeza.

    Katuga: Alielekeza au hakuelekeza njia ya kukinukisha?

    Brenda: Alielekeza.

  • Jaji: Tuendeleee

    Katuga: Kwa jina langu nitakuwa sahihi nikisema wewe ni mnyawezi mwenzangu

    Brenda: Ndio

    Katuga: Waambie majaji kama ulikuepo siku ya kupiga kura na ulikua wapi

    Brenda: Nilikuwepo nyumbani basi haya

    Katuga: Una cheo gani kingine ndani ya chama?

    Brenda: Mimi Katibu wa BAWCHA mkoa wa Kinondoni

    Katuga: Waambie majaji kama ulikitaja cheo hicho

    Brenda: ililenga mabadiliko katika nyanja ya kisiasa

    Katuga: Waambie majaji kama katika hituba ya mwenyeki kama ni ushahidi wako kwamba uliona hiyo video

    Brenda: Ni kweli niliona hii video

    Katuga: Je, ni kweli uliona kwenye mtandao wa kijamii wa Jambo

    Brenda: Ni ni kweli

    Katuga: Uliangakia youtube ya Jambo TV

    Brenda: Nimesema mitandao ya kijamii twende na hiyo hiyo youtube

    Katuga: Waambie waheshimiwa majaji kama nikikusikia sahihi ukisema neno kukinukisha ni slang sio neno rasmi

    Brenda: Ndio nilisema

    Katuga: Nitakuwa sahihi nilisema slang ni lugha isiyo rasmi inayotumika na kundi kwenye jamii

    Brenda: Ndio kama hivyo utakuwa sahihi

    Katuga: Waambie majaji kama katika ushahidi wako ulisema maana yake na inatumika na kundi gani

    Brenda: Sikusema inatumika na kundi gani nilisema maana yake

    Kataga: Kama nitakuwa sahihi ulisema kukinukisha ni kufanya kitu kinukie vizuri au vibaya ni slan au lugha rasmi

    Brenda: Ni tafsiri

    Katuga: Kitendo cha kufanya kitu kinukie kinaitwaje

    Brenda: Kukifanya kinukie

    Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema nimekinukisha

    Brenda: Utakuwa sahihi

    Katuga: Kwa kuwa hujataja ni kundi gani wanatumia hiyo slang nitakuwa sahahi nikisema inatumika na vijana wenu

    Brenda: Utakuwa sahihi

    Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema mtu akisema anaenda kukinukisha anaenda kufanya jambo lisilo la kawaida

    Brenda: Sijui

    Jaji: hilo litakuwa swali la mwisho

    Katuga: Ukisema raisi wa Jamuhuri ya Muungano hajatajwa kwenye hotuba ya mwenyekiti

    Brenda: ndio

    Katuga: Mheshimiwa jaji umenielekeza hilo ni swali la mwisho

    Jaji: Tuna ahirisha mpaka kesho saa tatu asubuhi kesho tuwahi

    Katuga: Kuna nyaraka mshitakiwa aliomba zimeshapitiwa naomba apokee

    Lissu: Hawa watu wananipa nyaraka zangu kama kina nani sababu hawa ndio wananishitaki

    Jaji: Kwa hiyo unazihitaji?

    Lissu: Niliomba maana yake nazihitaji

    Jaji: Naomba hizo nyaraka mshitakiwa apewe

    Katuga: Nina maswali yasiyopungua hamsini na hayajirudii na nikiangalia ni saa kumi na moja kamili

    Jiji: Wewe anza tunafidia dakika tano tulizopoteza asubuhi na tunafidia nusu saa tuliyopoteza asubuhi.

    Job: Kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa kuna mahali sheria hiyo inaruhusu kuvuruga uchaguzi?

    Brenda: Sijui

    Job: Kwa kuwa kwenye majibu yako umeeleza mahakama unaunga mkono maneno yote yaliyoko kwenye hati ya mashitaka kitendo hicho ni ukiukwaji wa katiba ya Chadema

    Brenda: Utakuwa hauko sawa

    Job: Kwa lugha nyingine kama sio sahihi unawaeleza majaji swala la kuvuruga uchaguzi kukinukisha kama lilivyosemwa na mshitakiwa msingi wake ni ibara ya tatu tatu moja ya katiba ya chadema

    Brenda: Wingi wake unatokana na msimamo wa chama

    Brenda: Msingi wake unatokana na msimamo wa chama

    Job: Msingi unatokana na ibara ya tatu moja tatu

    Brenda: Ndio unatokana na ibara hiyo

    Job: Umetoa tamko lolote kuhusiana na mwenendo wa kesi hii

    Brenda: Sikumbuki

    Job: Una shida ya kumbukumbu?

    Brenda: Hapana nimetoa matamko mengi ila sio specific kwenye kesi hii licha ya kwamba nimekuwa nikitoa maoni yangu juu ya mwenyekiti kuendelea kushikiliwa sababu ya nia ovu ya serikali

    Job:Ulitoa hayao kupitia wapi

    Brenda: Kupitia simu yangu na mitandao ya kijamii

    Job: Ulikuwa unazungumza na nani

    Brenda: Ukiwa mtandaoni uzungumza mbele ya kamera ya simu yako

    Job: ila ulitaka umma wa watanzania wafuatilie na wajue

    Brenda: Ndio

    Job: Ilikuwa lini

    Brenda: Sikumbuki ilikuwa lini

    Job: ilikuwa mwaka gani

    Brenda: Kati ya mwaka huu na mwaka jana

    Job: Una fahamu kutokujua sheria hakuondoi kosa

    Brenda: Ndio

    Job: Unafahamu jinai haifi

    Brenda: ndio

    Job: utakubaliana na mimi tamko hilo ulilotoa ni kinyume cha sheria za nchi

    Brenda: Hapana

    Job: Naomba nishie hapa wenzangu waendelee

    Job: Shahidi nina maswali machache…Kama nilikusikia vyema ulishiriki kwenue ule mkutano wa tarehe tatu april 2025

    Brenda: Ndio nilishiriki

    Job: Nataka uwaambie majaji mwenyekiti wa chama Tundu Lissu wakati anaongea na hadhara alipotamka haya maneno uliyosomewa hapa aliungwa mkono hakuungwa mkono?

    Brenda: Sijui

    Job: Umeiambia mahakama ulikuepo

    Brenda: Ndio nilikuepo

    Job: Hebu iambie mahakama hii majukumu yako mahususi

    Brenda: Ni pamoja kusimamia itifaki kwenye mikutano ya ndani na ya hadhara iwapo Katibu Mkuu anakuwa hayupo

    Job: Swali linaweza kuwa pana tuliweke hivi kwenye hiyo sehemu ya mawasiliano kazi yako nini

    Brenda: Waheshimiwa Majaji kuhusiana na mawasiliano huwa na ratibu pale chama kinapohitaji waandishi wa habari ambao kupitia kwao chama kinawasiliana na umma.Lakini pia mimi ninasimamia utendaji wa kazi unaofanywa na watu chini yangu

    Job: nitakuwa sahihi nikisema wewe sio Afisa Mawasiliano ni afisa mualikaji

    Brenda sio sahihi mimi nasimamia idara yote

    Job: Watu walioko chini yako wanafanya nini kuhusiana na mawasiliano

    Brenda: Wana alika waandisha wa habari wanawasiliana na viongozi wanawasiliana na umma kupitia vyombo vya habari. Wanataoa matangazo kwa niaba ya kurugenzi ya mawasiliano ya chama

    Job: Kwa hicho ulivhosema ni sahihi kuwa moja ya jukumu lako ni kuhabarisha umma

    Brenda: Ndio ni sahihi

    Job: Utakubaliana na mimi kwamba moja ya sheria katika nchi hii inayosimamia maswala ya habari ni media service act

    Brenda: Ndio

    Job: Ukiwa kama mkurugenzi wa mawasiliano umesoma

    Brenda: Ndio

    Job: Inatumika na nani

    Brenda: Watu walioko chini yangu

    Job: Waambie majaji wewe umesoma nini

    Brenda: Accounting

    Job: Huna elimu kuhusiana na mambo ya habari na wewe sio mwandishi wa habari

    Brenda: Hapana sijasomea uandishi wa habari

    Job: Ndugu shahidi umewahi kusikia neno kishoka

    Brenda: Sijawahi kusikia kwa kingereza ni nini

    Job: Utakubaliana na mimi kwamba mtu yeyote anayefanya kazi ya kutoa huduma ya habari na hana sifa za kutoa hiyo kwa mujibu wa sheria anakiuka maadili ya habari?

    Brenda: Sijui

    Job: Ni sahihi unawaeleza majaji ukiwa unafanya kazi Chadema ya kuhabarisha umma huitaji kuwa na sifa zilizo ainishwa kwenye sheria kwamba yeyote yule sheria hii haimuhusu

    Job: Sasa jibu swali

    Brenda: Rudia swali

    Job: Ni sahihi kwamba mtu yeyote ambaye hana sifa za kutoa huduma ya habari anaweza kufanya kazi kwenye idara ya mawasiliano Chadema?

    Brenda: Sio sahihi

    Job: Kama nimekusikia vizuri ukisema taaluma ya habari sio hitajio kwenye hiyo idara

    Brenda: Sio sahihi

    Job: Kama sio sahihi wewe ambaye unafanya kazi pale unafanya kazi kikamisa na hujui chochote

    Brenda: Sio kweli kwamba sijui chochote na siko peke yangu niko na idara

    Job: Nakuuliza wewe

    Brenda: Sio sahahi relax Job

    Brenda: Wewe ndo relax mbona unapata hasira ghafla

    Job: Tukisema mtu asiye na sifa ya kutoa uandishi wa habari ni kanjanja

    Brenda: Sifahamu

    Job: Ni sahihi umekuwa mwanachama wa Chadema kwa muda sasa

    Brenda: Ndio nimekuwa mwanachama tangu mwaka 2013

    Job: Nitakuwa sahihi nikisema wewe …Brenda Rupia unaifahamu vyema Chadema

    Brenda: Ndio

    Job: Nini ni falsafa ya Chadema

    Brenda: Chadema inaamini katika nguvu ya umma

    Job: hiyo nguvu ya umma imetafsiriwa vipi kwenye katiba yenu

    Brenda: Waheshimiwa majaji sio vizuri sana kukariri vifungu lakini ni kushirikisha umma mambo yake ikiwa chaguzi na kushirikisha umma katika matukio katika maamuzi

    Job: Hayo unayofafanua yameandikwa kwenye katiba

    Brenda: Ni tafsiri yangu mimi kama brenda

    Job: Nitakuwa sahihi nikikuambia wewe Brenda huijui vyema falsafa ya Chadema?

    Brenda: Utakua hauko sahihi

    Job: Kwa sababu umepatia au nimekosea

    Brenda: Utakua hauko sahihi

    Job: Nitaomba shahidi atusomee ibara ya tatu ya chama chao niweze kumuuliza maswali

    Brenda: Falsa ya chama ni kuamini katika nguvu ya umma

    Job: Soma tatu moja tatu

    Brenda: anasoma …………..

    Job: Swali umeelewa sawa hiyo ibara

    Brenda: Ndio nimeelewa

    Job: Unaelewa kwamba nchi hii ina katiba

    Job: Wewe kama Brenda ulimuunga mkono wakati anatamka yale maneno

    Brenda: Ndio nilimuunga mkono

    Job: Kwa kukubaliana naye

    Brenda: Ninakubaliana naye na hata leo nakubaliana na hayo maneno

    Job: Ni sahahi kwamba ibara ya tatu moja tatu inaelekeza Chadema kulinda katiba ya Tanzania

    Brenda: Ni sahihi

    Job: Na utakubaliana mimi sheria ya uchaguzi hapa nchini Tanzania ni moja ya sheria iliyotungwa katika msingi huu wa kikatiba

    Brenda: Nakubaliana na wewe

    Job: Katika msingi huo swala la kuvuruga uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2025 ni ukikwaji wa katiba ya nchi?

    Brenda: Sijui

    Job: Hebu isaidie mahakama waambie majaji kabla ya uchaguzi mkuu ufanyike ni sahihi kwamba Tume ya Uchaguzi imekuwa na utaratibu wa kutoa kanuni ya maadili ya wanasiasa yanayopaswa kuasainiwa

    Brenda: Ni sahihi

    Job: Wewe ukiwa kama mwenezi chadema ilisaini hizo kanuni mwaka 2020

    Brenda: Sikumbuki

    Tawabu: Uliposema ameshitakiwa kwa uongo unadanganya

    Brenda: Shitaka ni la uongo

    Tawabu: Imo au haimo kwamba alichapisha jambo

    Brenda: Hilo halimo jambo tv haijatajwa kwenye hati ya mashitaka

    Tawabu: Kuna watu uliwataja wako kwenye sekretarieti

    Brenda: Sikumtaja John Heche kwenye sekretarieti

    Tawabu: Ulisema maudhui ni mali ya chombo husika cha habari

    Brenda: Nilisema mmliki wa maudhui ni chombo husika cha habari na. mmliki namba moja atakuwa mkurugenzi wa chombo husika

    Tawabu: Diamond, Mbosso na Mario una wafahamu?

    Brenda: Nawasikia

    Tawabu: Wanajihusisha na nini?

    Brenda: Ni wanamuziki

    Tawabu: Kwa hiyo anachokisema Tundu Lissu kupitia Jambo TV sio cha kwake?

    Brenda: Ndio sio cha kwake

    Tawabu: Uliulizwa haya maneno yaliyoko kwenye hati ya mashitaka ni kosa sio kosa

    Brenda: Sio kosa

    Tawabu: Unakumbuka tafsiri ya uasi nakuopa kamusi utusomee tena

    Brenda: Kitendo cha kuwapinga wenye mamlaka..Kitendo cha uvunjaji wa sheria kinachofanywa na kikundi cha watu wanaotaka kuziondoa mamlaka za nchi yao

    Tawabu: Kwenye maneno ya huyu bwana neno uasi lilikuwpo halikuepo

    Brenda: Lilikuepo

    Tawabu: Ulisema kwamba kufanya kitu kitoe harufu nzuri au mbaya sio kosa

    Brenda: Sio kosa

    Tawabu: Ukifuga kuku wakatia harufu mbaya sio kosa au ni kosa

    Brenda: Sioni kama nin kosa waheshimiwa Majaji

    Tawabu: Kuna kifungu kwenye pino kodi kinaongelea kutoa harufu mbaya je huoni unakinzanza na sheria

    Brenda: Mimi sijui nifafanulie hiyo sheria

    Tawabu: Nikikuambia kuna sheria inazuia watu wasitoe harufu mbaya utakubaliana na mimi

    Brenda: Nisomee hiyo sheria mimi siwezi kukubali

    Tawabu: Wewe ni mtaalamu wa hesabu

    Brenda: Nimesomea account

    Tawabu: Mtu akisema asilimia ina maanisha nini

    Brenda: Ndio

    Tawabu: Ukisema asilimia kubwa una maanisha nini

    Brenda: Ni zaidi ya asilimia hamsini

    Tawabu: Na hukufafanua

    Brenda: Ndio sikufafanua

    Tawabu: Hawa zaidi ya asilimia hamsini ni wakina nani

    Brenda: siwakumbuki

    Tawabu: Kuna mahala ulisema tarehe kumi mwezi wa sita kwengine tarehe 17 ulikuwa unatumia kalenda gani

    Brenda: Nilikuwa ninamaanisha tarehe niliyoitaja

    Tawabu: Ulikuwa unamaanisha aina gani ya kalenda

    Brenda: Sijui aina ya kalenda

    Tawabu: Ulipokuwa unatoa ushahdi ulirudia sana mwenyekiti wa chama mkurugenzi wa chama hapa Tanzania kuna vyama vingapi vya kisiasa

    Brenda: Nasikia viko 19

    Tawabu: Unaweza kututajia hata viwili

    Brenda: Chadema, ACT, Chauma

    Tawabu: Ulikuwa unasema mkuregenzi wa chama na hukusema chama gani

    Brenda: Waheshimiwa Majaji nilipoanza kujieleza nilisema mimi ni Mkurugenzi Mawasiliano na Uenezi Chadema

    Tawabu: unakubali kwamba ulisema chama ila hukussema chama gani

    Brenda: Ndio

    Tawabu: Umetuambia wewe ni mkurugenzi wa mawasiliano na uenezi

    Brenda: Ndio

    Tawabu: Unaposema mshitakiwa sio mfanyakazi wa Jambo TV kwa nafasi yako unaweza kujua?

    Brenda: Hapana siwezi kujua

    Tawabu: Umetuambia kwamba neno uasi ilitokana na kauli ya G55 hao G55 waliongea wakati gani kwenye mkutano wenu

    Brenda: Hawakuongea alikuwa anajibu waraka wao

    Tawabu: Unakubaliana na mimi mahakama hii ni ya kisheria na sio kihisia

    Brenda: Ndio ninakubalina

    Tawabu: Ulisema umekamatwa na polisi lakini haujawahi kupelekwa mahakamani hivyo unaombaia mahakama uko tayari kama mambo yako yamekubalika

    Brenda: Kama wanaona kama wanamashitaka niko tayari

    Tawabu: Ni hayo tu waheshia majaji

    Tawabu Issa Tawabu: Naomba utusomeee neno haki kwenye kamusi

    Brenda: anasoma ……..

    Tawabu: Kwa hiyo hapo kamusi inasema haki ni kumpa mtu kile anachostahili

    Brenda: Hiyo ni definitation moja

    Tawabu: Huyu mwamba anashitakiwa kwa kukika kifungu cha 39 cha kanuni ya adhabu hiyo nakupa taarifa sasa kanuni ya adhabu ni sheria na mahakama inasimamia haki na hilo lipo kikatiba.

    Brenda: Ndio

    Tawabu: Uliposema huyu bwana hajatenda makosa ulitoa wapi hayo mamlaka ya kusema hivyo

    Brenda: Mamlaka ndio yenye kauli ya mwisho

    Tawabu: Wewe hayo mamlaka unayo

    Brenda: Mamlaka ya kutoa kauli ya mwisho ni ya mahakama

    Tawabu: Umeulizwa sana kuhusu maneno aliyosema mshitakiwa umewahi kuelewa maana ya uhaini ni nini

    Brenda: Ni kuisaliti nchi yako kutaka kupindua serikali huo ndio uelewa wangu wa uhaini

    Tawabu: Kwa kuwa umetuambia tafsiri yako ya uhaini kwa uelewa wako wa kawaida na kukiwa na tafsiri nyingine inayoweza kuthibitishwa na Mahakama na mtu akatendewa haki huna shida.

    Brenda: Ndio

    Tawabu: Umeulizwa sana kuhusu uasi kamusi ya kiswahili inasemaje kuhusu uasi

    Brenda: Kitendo kinachofanywa na kikundi cha watu kubadili mfumo wa nchi yao bila kufuata sheria

    Tawabu: Hivyo ni sahihi tafsiri ya uasi ndio hiyo

    Brenda: Nitaenda na B

    Tawabu: Kwa hiyo uasi ni kuvunja sheria

    Brenda: Ni sahihi kwa moja ya fasiri

    Tawabu: Nchi yetu ni ya kisheria au inaendeshwa kiimla

    Brenda: kiimla

    Tawabu: Na kinachofanyika hapa Mahakamani

    Brenda: Haya ni ya kimahakama

    Tawabu: Uliambia mahakama una uwezo wa kufanya miujiza

    Brenda: Hapana

    Tawabu: Uliposema ulipanda gari halina milango ulioandaje

    Brenda: Hiyo humaan error

    Tawabu: kwahiyo unedanganya

    Brenda: Hapana magari ya mapolisi yako wazi

    Tawabu: Uliposafirishwa na pro boxx uliwekwa wapi

    Brenda: Nyuma

    Tawabu: Walikutesa sana

    Brenda: Sijasema

    Tawabu: Nyuma ulikaa upande gani

    Brenda: Nyuma Kushoto

    Tawabu: Mlikuwa watu wangapi

    Brenda: Watu watatu Jaji kwa maana ya wasijulikana wawili

    Brenda: Ndio mheshimiwa Jaji

    Tawabu: Nitakuwa sawa sawa nikisema ushahdi uliotoa hauhusiani na kesi hii

    Brenda: Sijui

    Tawabu: Hati yako ya kusafiria ina husiana na kesi ya mwenyekiti ya kukinukisha?

    Brenda: Ilikuwa ni mwendelezo wakuonesha namna namna watawala wanavyokandamiza viongozi wa Chadema

    Tawabu: Jibu swali

    Brenda: Nareja ni mwelezo wa ukandamizaji

    Tawabu: Kuna sehemu passport yako imeandikwa tutahamasisha uasi

    Brenda: Nimesema ni mwendelezo wa ukandamizaji. wa raia

    Tawabu: Uongo ni nini

    Brenda: Mwenyekiti sio mhaini shitaka lake ni la uongo

    Tawabu: Kwa mujibu sheria shitaka lipo au lipo.

    Brenda: Shitaka ni la uongo.

    Cuthbert Mbiling’i: Yale maneno ya kwenye hati ya mashitaka hayana ubishani kwamba alisema mwenyekiti

    Brenda: Ni kweli aliyasema

    Cuthbert: Mi kweli alisema uasi

    Brenda: Alisema

    Cuthbert: Tutakinukisha

    Brenda: Tutakinukisha kweli kweli

    Cuthbert: Unafahamu anashitakiwa na nini

    Brenda: Hayo maneno kuwa ni uasi

    Cuthbert: Umesema hayo sio makosa

    Brenda: Ndio sio makosa

    Cuthbert: Waambie majaji kwa mujibu wa sheria ipi

    Brenda: Sijui kuhusu sheria

    Cuthbert: Waambie majaji hayo ni maoni

    Brenda: Ni fact

    Cuthbert: Ulikamatwa Namanga na hukuIambia Mahakama ulikamatwa kwanini

    Brenda: Waliniambia ni sababu ya taarifa niliyotoa

    Cuthbert: Unajua kwamba jinai haiozi

    Brenda: Nafahamu

    Cuthbert: Kwa hiyo wakitaka kukupeleka mahakamani

    Brenda: Wakiona inafaa

    Cuthbert: Umesema ulikamatwa na mtu mwingine

    Brenda: Nilikamatwa na nilimuona leonard magere mahabusu

    Cuthbert: Taarifa ya kukamatwa kwako umeileta mahakamani

    Brenda: Hapana

    Cuthbert: Tangu unajiunga Chadema una miaka zaidi ya kumi. Je nafasi uliyo nayo muhusika anapatikanaje

    Brenda: Nimejiunga Chadema mwaka 2013 na nimeshika nafasi mbali mbali na kumteua mkurugenzi wa mawasiliano kuna mchakato wa kikatiba unafuatwa

    Cuthbert: Na huwezi kuchaguliwa kama sio mwanachama wa Chadema

    Brenda: Ni sahihi

    Cuthbert: Unafahamu nani alikupendekeza

    Brenda: Sifahamu

    Cuthbert: Unakubaliana na mimi kwamba ni mmoja wa viongozi wa chama

    Brenda: Ndio

    Cuthbert: na utakubaliana mimi utendaji wako wa kazi unarIpoti kwa katibu mkuu na viongozi wengine wajuu

    Brenda: Ninatoa taarifa kwa sekretarieti ya Chama

    Cuthbert: Unapofanya nakisa ya kiutumishi unawajibishwa na nani?

    Brenda: Kamati kuu

    Cuthbert: Na ni sahihi kwamba 20/8/2026 kamati kuu walikaa kikao

    Brenda: Ndio sikumbuki tarehe lakini ila ni juzi juzi tu hapa

    Cuthbert: Na moja kati ya maazimio ya kikao ilikuwa kumtetea mwenyekiti kwa nguvu mahakamani

    Brenda: Sio shahihi

    Cuthbert: Akitokea mtu mwingine akasema hivyo nani atakuwa maeidanganya mahakama

    Brenda: Huyo mtu mwingine atakuwa amaeidianganya mahakama Cuthbert: Ni wajibu wako kufata maelekezo ya viongozi wako wa chama

    Brenda: Ni sahihi

    Cuthbert: Ulishwahi kutoa ushahidi wowote dhidi ya kiongozi yeyete wa Chadema dhidi yake sio kumetetea

    Brenda: Sijawahi

    Cuthbert: Na kuhusu kumtetea mwanachama au kiongizi wa chama mahakamani?

    Brenda: Hii ndio mara ya kwanza Cuthbert na nikisema wewe ni shahidi mwenye interest sio shahidi huru

    Brenda: Mimi ni shahdi mwenye interest ya haki kutendeka

    Cuthbert: Utakubaliana na mimi ushahidi wako uchukuliwe kwa tahadhari sababu una interest

    Brenda: Sijui

    Cuthbert: Jana ukisema mshitakiwa sio mmiliki wa jambo tv wala hizo content zilizorushwa

    Brenda: Ndio

    Cuthbert: Una ushahidi wa kuthibitisha hilo

    Brenda: Sijaleta waheshimiwa majaji

    Cuthbert: Waheshimiwa majiji naomba niishie hapo.

    Winniwa: Maana ya kuvuruga uchaguzi umesema sio kosa

    Brenda: Sio kosa

    Winniwa: Unafahamu uchaguzi uko kisheria

    Brenda: Uchaguzi huru na wa haki

    Winniw: Chaguzi zote ziko kisheria

    Brenda: Ziko kwa mujibu wa sheria

    Winniwa: Je mtu akitaka kuvuruga uchaguzi anavunja sheria

    Brenda: Sio kweli

    Winniwa: Sawa kwa uelewa wako lakini

    Winniwa: Ulisema ulikuwa unaenda mafunzo Ujerumani je umeleta uthibisho hapa mahakamani unakwenda nje kwa mafunzo

    Brenda: Sijaleta

    Winniwa: Ni sahini hujawahi pelekea malalamiko yako yoyote kwa kushikiliwa na kunyang’anywa hati yako ya kusafiri

    Brenda: Sijasema kitu kama hicho

    Winniwa: Hujaileza mahakama ulivyochaguliwa kuwa mkurugenzi wa mawasiliano:

    Brenda: Sikuulizwa

    Winniwa: Unafahamu nini maani ya neno uasi

    Brenda: Kupinga kukataa kwa nguvu kubwa

    Winniwa: Kwa hiyo mwenyekiti aliposema uasi alimanisha atatumia nguvu kubwa

    Brenda: Aijasema manguvu kubwa nimesema kupinga na kukataa kwa nguvu kubwa sio kwa manguvu makubwa

    Winniwa: Unaelewa nini unaposikia kukinukisha

    Brenda: Kunukia au kunuka vibaya

    Winniwa: Kwa hiyo mlitaka nini kinukie

    Brenda: Ukipika pilau kika mtu atajua unapika pilao hivyo tukipinga kwa nguvu kila mtu atajua tunapinga

    Winniwa: Waheshimiwa majaji ninaishia hapa nina waaliaka wenzangu waweze kuendelea.

    STORI NA DENIS MTIMA | GPL -MAHAKAMANI

Leave a Comment