×

Libasse Gueye Mchezaji Bora Agosti, Manqoba Kocha Bora Ligi Kuu

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Libasse Gueye, ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Agosti wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/27, huku kocha wa Young Africans, Manqoba Mngqithi, akichaguliwa kuwa Kocha Bora wa Mwezi huo.

Gueye alionesha kiwango kizuri katika mwezi huo, akishinda tuzo hiyo mbele ya Maxi Nzengeli wa Young Africans na Oscar Mwangaja wa Mbeya City.

Katika michezo mitano ambayo Simba ilicheza mwezi Agosti, Gueye alitoa mchango mkubwa kwa timu yake, iliyoshinda michezo yote mitano na kufunga bao moja kati ya mabao yaliyofungwa na Simba katika kipindi hicho.

Kwa upande wa Manqoba Mngqithi, kocha huyo aliiongoza Young Africans kushinda michezo yote mitano iliyocheza mwezi Agosti, hivyo kuiweka timu hiyo kileleni mwa msimamo wa ligi.

Kocha wa Yanga, Manqoba Mngqithi Kocha Bora wa Mwezi.

Wakati huo huo, Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemtangaza Meneja wa Uwanja wa Bukombe, mkoani Geita, Deogratius Dayan, kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Agosti.

Tuzo hiyo imekuja kutokana na namna alivyofanya vizuri katika usimamizi wa matukio ya michezo pamoja na kushughulikia masuala mbalimbali yanayohusu miundombinu ya uwanja.

Aidha, Kamati hiyo imeteua mabao matatu yaliyofungwa katika mwezi Agosti kuwania Bao Bora la Mwezi. Mabao hayo ni la Shekhan Hamis (Singida BS dhidi ya Polisi Tanzania), Robert Mathias (Geita Gold dhidi ya Kagera Sugar) na Hija Shamhe (Mbeya City dhidi ya Mashujaa).

 

Leave a Comment