×

Simba Yapoteza Mechi ya Pili Mfululizo Afrika Kusini

Klabu ya Simba SC imepoteza mchezo wake wa pili mfululizo wa kirafiki nchini Afrika Kusini, baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Sekhukhune United.

Mchezo huo ulikuwa wa pili kwa Simba katika kambi yao ya siku 10 nchini Afrika Kusini na umehitimisha kambi hiyo, huku timu hiyo ikiendelea na maandalizi ya msimu mpya.

Kipigo hicho kinakuja siku moja baada ya Simba kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Polokwane City, katika mchezo mwingine wa kirafiki nchini humo.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kumaliza kambi ya Afrika Kusini bila kupata ushindi katika michezo yake miwili ya kirafiki, huku benchi la ufundi likitumia michezo hiyo kuwapima wachezaji na kuendelea kujiandaa kwa mechi za msimu ujao.

Simba sasa inaelekeza nguvu kwenye maandalizi ya mechi zake zijazo, ikiwemo Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga inayotarajiwa kuchezwa Oktoba 10.

Leave a Comment