MISRI: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi, amekutana na Rais wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha New Alamein nchini Misri.
Ndejembi yuko nchini Misri kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Nane wa Kamati ya Uratibu ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (8th African Union Mid-Year Coordination Summit).

Mkutano huo unawakutanisha viongozi wa Afrika kujadili masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa ajenda za Umoja wa Afrika, ushirikiano wa kikanda na masuala yenye maslahi kwa bara la Afrika.
Katika ziara hiyo, Makamu wa Rais anawakilisha Tanzania katika mkutano huo muhimu unaolenga kuimarisha uratibu na utekelezaji wa mipango ya Umoja wa Afrika na jumuiya za kikanda.
