
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya viwanja kwa ajili ya mazoezi ya timu siku moja kabla ya mechi, ikisisitiza kuwa hakuna kanuni inayozuia timu kutumia uwanja kwa ajili ya mazoezi hayo.
Katika taarifa iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Cornel L. Barnabas, imeelezwa kuwa kanuni za timu ngeni kutumia uwanja kwa ajili ya mazoezi siku moja kabla ya mechi zilifutwa katika marekebisho ya Kanuni za Ligi Kuu yaliyoipitishwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa msimu wa 2026/2027.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa kutokana na marekebisho hayo, hakuna kanuni inayoruhusu timu kutumia viwanja kwa ajili ya mazoezi kabla ya mechi, hata timu mwenyeji.
Kwa mujibu wa TPLB, lengo la kufuta kanuni hiyo ni kuhakikisha viwanja vinakuwa tayari na katika ubora unaotakiwa kwa ajili ya mechi za ligi.
Taarifa hiyo imesainiwa na Cornel L. Barnabas kwa niaba ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania.
