
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Camillus Wambura, amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Matride Kuyeto, kutoka Kamanda wa Polisi Kikosi cha Reli na kumteua kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida (RPC).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Oktoba 13, 2026, ACP Kuyeto anachukua nafasi ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Amon Kakwale, ambaye amestaafu utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria.
Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Makao Makuu ya Polisi, Dodoma.
