MAJIBU YA MITIHANI, MAJARIBIO MENGI YA NDANI
Mwanafunzi, leo nitamalizia mada hii niliyoianza wiki iliyopita lengo likiwa kukupa ufahamu zaidi kuhusu suala la kujiandaa na kufaulu mitihani.
Kitu kingine ambacho wanafunzi hupaswa kujipima nacho ni kwa kupitia matokeo ya mitihani na majaribio mengi yanayotolewa na walimu wao, hapa wakijipima kwa idadi ya alama wanazopata ambapo alama zao zinapozidi hicho huwa ni kipimo cha uelewa wao na utayari kwa ajili ya mitihani.
USAHIHI WA MAJIBU YAKO DARASANI
Kipimo kingine huwa ni usahihi wa majibu wayatoayo wanafunzi pindi mwalimu anapouliza swali darasani. Mwanafunzi anaweza kupima uelewa wake na utayari wa kuingia kwenye chumba cha mtihani kwa njia hii.
Usikose wiki ijayo kwa mada nyingine.