×

Tanasha Donna Aanza Mpango Mpya wa Kutikisa Mitandao Kupitia “Tea”

Mwimbaji na mwanamitindo maarufu kutoka Kenya, Tanasha Donna, amewashukuru mashabiki wake kwa kuendelea kuusikiliza na kuusambaza wimbo wake mpya “TEA”, huku akidokeza kuja kwa challenge inayotarajiwa kuufanya wimbo huo kuendelea kutamba mitandaoni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Tanasha ameeleza kufurahishwa na upendo ambao mashabiki wameuonesha kwa wimbo huo tangu ulipotoka, akiwataka kuendelea kuusikiliza, kuushirikisha na kuupa sapoti.

“Ninashukuru sana kwa upendo wote ambao mmetuonesha kwa TEA hadi sasa. Endeleeni kuusikiliza, kuushirikisha na kuonesha upendo kwa TEA, kwa sababu ndio kwanza tumeanza,” ameandika Tanasha.

Katika ujumbe huo, msanii huyo pia amewapa mashabiki wake hamasa zaidi baada ya kutangaza kuwa challenge ya wimbo huo inakuja hivi karibuni, huku akiwauliza kama wako tayari kushiriki.

“Challenge inakuja hivi karibuni… je, mpo tayari?” ameongeza.

Tangazo hilo linaashiria hatua nyingine katika juhudi za Tanasha za kuutangaza wimbo huo na kuwashirikisha mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii, ambako challenges za muziki zimekuwa njia mojawapo ya kuongeza ushiriki wa mashabiki na kusambaza nyimbo kwa hadhira pana.

Tanasha amehitimisha ujumbe wake kwa kuwashukuru mashabiki kwa kuendelea kuwa naye katika safari yake ya muziki, akisisitiza kuwa anawapenda na kuthamini sapoti yao.

Sasa macho na masikio ya mashabiki yanaelekezwa kwenye challenge hiyo inayotarajiwa kutangazwa hivi karibuni, huku wakisubiri kuona ubunifu utakaotumika kuufanya wimbo “TEA” kuendelea kupata umaarufu.

Leave a Comment