
Xiaomi leo imezindua toleo la REDMI Note 17, kizazi kipya cha mfululizo wake wa simu janja unaouzwa zaidi, ikiwasilisha matoleo mapya mawili , ikiwemo muundo wa kwanza kabisa wa Pro Max ‚ REDMI Note 17 Pro Max 5G na REDMI Note 17 4G . Mfululizo huu unakuja na betri kubwa zaidi na kuchaji kwa haraka zaidi kwa matumizi ya muda mrefu, uwezo ulioboreshwa wa kustahimili maji na kuanguka, REDMI NOTE 17 inakuja na uimara wa kudumu katika kundi la simu za bei ya kati na kutimiza dhamira ya REDMI ya kuwa na simu janja “iliyojengwa kudumu kwa miaka mingi”
Uzinduzi huu pia unaashiria hatua kubwa Matoleo REDMI Note sasa umevuka usambazaji wa simu milioni 500 duniani kote,Kizazi baada ya kizazi, mfululizo huu umeendelea kushikilia kile kilichojenga imani hiyo “bidhaa bora zinazofikika kwa urahisi, na ubora katika kila bidhaa.” , Wateja watakonunua Simu hizi watapata ofay a GB 96 Bure kwa mwaka mzima, saa (smartwatch) REDMI 6 active kwa REDMI 17 na zawadi ya Headset Neo kwa REDMI NOTE 17 Pro max.
REDMI Note 17 Pro Max 5G, muundo wa kwanza kabisa wa aina yake, Ubora wa REDMI Titan na betri kubwa zaidi ya Xiaomi kuwahi kutengeneza ya 10,000mAh. Ukiwa pamoja na REDMI Note 17 Pro 5G, REDMI Note 17 4G, mfululizo huu wa vifaa vinne unawaletea watumiaji falsafa ya REDMI ya “Kujengwa Kudumu kwa Miaka” kulingana na mahitaji na mitindo tofauti ya maisha ya digital.
Matoleo haya huu unaonyesha dhamira ya Xiaomi ya kutengeneza simu janja zinazoendelea kutegemewa hata baada ya miaka mingi ya matumizi ya kila siku. Dhamira hiyo inaendelea katika kipindi chote cha umiliki wa kifaa, ikiwa na “Updates” za usalama kwa hadi miaka sita kwa matoleo yote mzima, watumiaji pia wananufaika na afya ya betri kwa hadi miaka sita. REDMI Note 17 Pro Max 5G inaenda hatua zaidi kwa kutoa uzoefu wa programu “kama mpya” kwa miaka sita.
Toleo la REDMI Note 17 linakuja na Mfumo wa Betri wa REDMI Titan, ulioundwa kwa teknolojia ya kisasa ya betri ya silicon-carbon ili kutoa mafanikio mawili makubwa kwa pamoja: maisha marefu ya betri na usimamizi wa akili wa matumizi ya nishati.
Ubora wa REDMI Titan umejengwa kwenye uzoefu ambao watumiaji hutegemea zaidi kila siku, kuanzia uimara wa betri. REDMI Note 17 Pro Max 5G inaleta betri kubwa zaidi ya Xiaomi kuwahi kutengeneza, yenye uwezo wa 10,000mAh na asilimia 16 ya kiwango cha silicon.