×

Picha 17: Muonekano wa Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma, Wazinduliwa Kwa Kishindo!

Muonekano wa majengo ya Ofisi za Wizara na Taasisi za Serikali pamoja na barabara za lami katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, kufuatia uzinduzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Oktoba 30, 2026.

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Samia amesema Serikali inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya kuendeleza Jiji la Dodoma kwa kuboresha miundombinu ya barabara, upatikanaji wa maji safi na salama, huduma za afya, elimu pamoja na upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Amesema uwekezaji huo ni sehemu ya jitihada za Serikali katika kuboresha huduma kwa wananchi na kuimarisha mazingira ya utendaji kazi wa Wizara na Taasisi za Serikali.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuyatunza majengo hayo na miundombinu mingine iliyojengwa, huku akihimiza usimamizi mzuri na kuzingatia usafi wa mazingira ili eneo hilo liendelee kuwa safi na lenye kuvutia.

Hatua hiyo inaendelea kuimarisha hadhi ya Dodoma kama Makao Makuu ya Serikali na kuifanya Mji wa Serikali Mtumba kuwa eneo muhimu la shughuli za kiutawala nchini.

Leave a Comment