×

Mabula Aapishwa Kuwa RC wa Tabora Ikulu ya Chamwino, Dodoma – Video

Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimuapisha Ndugu Angelina Lubala Mabula kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma, tarehe 02 Novemba, 2026.

Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimuapisha Ndugu Danford George Mpelumbe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma, tarehe 02 Novemba, 2026.
Dkt. Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimuapisha Jaji Mstaafu Wilfred Peter Dyansobera kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.
Rais Samia akimuapisha Ndugu Paul Thomas Kadushi kuwa Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.
Dkt. Samia akimuapisha Rifai Abdallah Mkumba kuwa Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.
Dkt. Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimuapisha  Kusirie Emmanuel Sinkondo kuwa Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Novemba 2, 2026, amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nafasi mbalimbali za uongozi serikalini na katika tume mbalimbali.

Uapisho huo umefanyika katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, ambapo miongoni mwa walioapishwa ni Angeline Lubala Mabula kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Dunford George Mpelumbe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Wengine ni Omar Ali Omar, aliyeapishwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, pamoja na Jaji Mstaafu Wilfred Peter Dyansobera, aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, sambamba na Makamishna wa Tume hiyo.

Leave a Comment