
Mwanasoka wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo, ameendelea kutawala ulimwengu wa michezo kwa upande wa mapato, akiongoza orodha ya wanamichezo wanaoingiza fedha nyingi zaidi duniani kwa mwaka 2026, kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Ronaldo, anayeichezea klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia, anakadiriwa kuingiza takribani Shilingi bilioni 793.5 za Tanzania kwa mwaka, kupitia mshahara wake wa soka, mikataba ya matangazo, udhamini na shughuli mbalimbali za kibiashara.
Katika nafasi ya pili yupo bondia wa Mexico, Canelo Álvarez, anayekadiriwa kuingiza Shilingi bilioni 449.7 kwa mwaka, huku mwanasoka Lionel Messi wa Inter Miami akishika nafasi ya tatu kwa mapato ya takribani Shilingi bilioni 370.3.

Nyota wa mpira wa kikapu wa Marekani, LeBron James, anashika nafasi ya nne akiwa na mapato ya Shilingi bilioni 364.5, akifuatiwa na mchezaji wa baseball wa Japan, Shohei Ohtani, anayekadiriwa kuingiza Shilingi bilioni 337.5 kwa mwaka.
ORODHA YA WANAMICHEZO 10 WANAOINGIZA FEDHA NYINGI ZAIDI DUNIANI
- Cristiano Ronaldo (Soka) – Shilingi bilioni 793.5.
- Canelo Álvarez (Ndondi) – Shilingi bilioni 449.7.
- Lionel Messi (Soka) – Shilingi bilioni 370.3.
- LeBron James (Mpira wa Kikapu) – Shilingi bilioni 364.5.
- Shohei Ohtani (Baseball) – Shilingi bilioni 337.5.
- Stephen Curry (Mpira wa Kikapu) – Shilingi bilioni 329.8.
- Jon Rahm (Gofu) – Shilingi bilioni 283.0.
- Karim Benzema (Soka) – Shilingi bilioni 275.1.
- Kevin Durant (Mpira wa Kikapu) – Shilingi bilioni 274.6.
- Lewis Hamilton (Formula 1) – Shilingi bilioni 264.5.
Kwa ujumla, orodha hiyo inaonesha namna sekta ya michezo inavyoendelea kuwa moja ya maeneo yenye mzunguko mkubwa wa fedha duniani, huku wanamichezo wakinufaika si tu na mishahara na zawadi za mashindano, bali pia mikataba ya matangazo, udhamini na uwekezaji wa kibiashara.