
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Beno Malisa, amemuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akieleza kuwa aliteleza katika utekelezaji wa majukumu yake wakati akihudumu katika nafasi hiyo.
Malisa ametoa kauli hiyo Novemba 3, 2026, wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora iliyofanyika katika Ukumbi wa Isike Mwanakiyungi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Malisa amekiri kuwepo kwa mapungufu katika utekelezaji wa majukumu yake na kumuomba radhi Rais Samia, huku akieleza kuwa amepokea uamuzi wa kumuondoa katika nafasi hiyo kwa heshima.
Malisa alitenguliwa katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Oktoba 28, 2026, na nafasi yake kuchukuliwa na Angelina Mabula, ambaye anatarajiwa kuendelea na majukumu ya kuongoza mkoa huo.