Benki ya NMB imepata mkopo wa dola za Marekani milioni 30 kutoka Benki ya Maendeleo ya China (CDB) kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa mitaji kwa biashara ndogo na za kati nchini Tanzania. Makubaliano hayo yametiwa saini katika Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam, yakilenga kuchochea ukuaji wa biashara na kuimarisha ushirikiano wa kifedha kati ya Tanzania na China.
Zaipuna amesema ushirikiano huo pia utaimarisha huduma za kifedha kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara na China. Kupitia mfumo wa CIPS, NMB inatoa huduma za malipo kwa sarafu ya China (RMB), akaunti za biashara na ufadhili wa biashara za kimataifa, huku ikiunganisha wafanyabiashara wa Tanzania na wazalishaji wa China kupitia maonesho ya Canton Fair.Makubaliano hayo yanafikiwa wakati NMB ikiwa imetambuliwa na jarida la Global Finance kuwa Benki Bora kwa Biashara Ndogo na za Kati Tanzania mwaka 2026. Mkopo huo unatarajiwa kuongeza fursa za mitaji kwa wajasiriamali, kuimarisha biashara kati ya Tanzania na China na kuunga mkono utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

.jpeg)
.jpeg)