Vodacom Yazindua M-Pesa Mchezo Kurahisisha Usimamizi wa Upatu Kidijitali
Hashpower7113 November 10, 2026 96 views 0 Comments
SHARE THIS:
Kaimu Mkurugenzi wa M-Pesa Vodacom Tanzania Tulisindo Mlupilo (kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki kwa Wateja Binafsi wa ABSA Bank Ndabu Lilian Swere, (katikati) na Mkurugenzi wa Afropavo Limited Rwebu Mutahaba wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa MCHEZO, huduma mpya ya kidijitali inayowawezesha Watanzania kusimamia vikundi vya upatu kupitia M-Pesa. Huduma hiyo imezinduliwa kupitia ushirikiano wa Vodacom Tanzania, ABSA Bank na Afropavo Limited, kwa lengo la kuimarisha uwazi, kurahisisha usimamizi wa michango na kuhakikisha wanachama wanapata taarifa za miamala ya vikundi vyao.
Huduma mpya ya kidijitali iitwayo MCHEZO imezinduliwa rasmi, ikiwa na lengo la kuwawezesha Watanzania kusimamia vikundi vyao vya upatu kwa njia rahisi, salama na ya uwazi zaidi kupitia M-Pesa.
Kaimu Mkurugenzi wa M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Tulisindo Mlupilo (wa nne kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki kwa Wateja Binafsi wa ABSA Bank, Ndabu Lilian Swere (wa tano kushoto) na Mkurugenzi wa Afropavo Limited, Rwebu Mutahaba (wa tano kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka kampuni hizo wakati wa uzinduzi wa MCHEZO, huduma mpya ya kidijitali inayowawezesha Watanzania kusimamia vikundi vya upatu kupitia M-Pesa. Uzinduzi huo umefanyika leo Novemba 10, 2026, kupitia ushirikiano wa Vodacom Tanzania, ABSA Bank na Afropavo Limited.
Huduma hiyo imezinduliwa kupitia ushirikiano kati ya Vodacom Tanzania, ABSA Bank na Afropavo Limited
Baadhi ya Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc pamoja na watengenezaji wa maudhui, wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa M-Pesa, Tulisindo Mlupilo, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa MCHEZO, huduma mpya ya kidijitali inayowawezesha Watanzania kuanzisha na kusimamia vikundi vya upatu kupitia M-Pesa. Huduma hiyo inawawezesha wanachama kuanzisha au kujiunga na vikundi, kuchangia fedha na kufuatilia michango pamoja na taarifa za miamala ya vikundi vyao.