×

Ndejembi Azuru Kaburi la Hayati Benjamin Mkapa Lupaso


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ametembelea kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa, lililopo Lupaso, Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.

Ziara hiyo imefanyika leo, Novemba 12, 2026, ambapo Makamu wa Rais aliambatana na familia ya Hayati Mkapa, viongozi wa dini pamoja na viongozi wa Serikali.

Akiwa katika eneo hilo, Makamu wa Rais pamoja na viongozi walioambatana naye wamefanya maombi maalumu katika kaburi la Hayati Mkapa na kuweka shada la maua kwa heshima ya kiongozi huyo aliyewahi kuliongoza Taifa katika Awamu ya Tatu.

Leave a Comment