×

Video: Wakili Aibua Mazito Chanzo Dereva wa Kijiko Kuharibu Majengo na Magari ya Mchina

Wakili wa Kampuni ya China Energy Engineering Group Guangxi Hydroelectric Construction Bureau Co. Ltd amezungumza na Global TV.

Kufuatia tukio la Khalid Seleman Kalaghe (45), dereva wa mashine ya kuchimbia ardhi (Excavator), kutuhumiwa kuharibu mali mbalimbali za mwajiri wake mwenye asili ya China baada ya kuibuka kwa mgogoro kati yao, Global TV imefika katika eneo la tukio kufuatilia kwa kina kilichojiri.

Akiwa eneo la tukio, Wakili wa Kampuni ya China Energy Engineering Group Guangxi Hydroelectric Construction Bureau Co. Ltd amezungumza na Global TV, akieleza undani wa sakata hilo, chanzo cha mgogoro pamoja na hatua zilizochukuliwa na kampuni hiyo hadi sasa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, tukio hilo lilitokea Novemba 10, 2026, majira ya saa 6:05 mchana, katika Mtaa wa Mvumoni, eneo la Somangila, Manispaa ya Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Leave a Comment