
Unatafuta bidhaa, unapanga safari au unasimamia biashara? Kika ni msaidizi wa akili mnemba (AI) wa KikaPay anayekuwezesha kupata huduma mbalimbali kupitia WhatsApp, bila kupakua programu nyingine.
Kutumia Kika ni rahisi: tuma ujumbe, picha au sauti kwa Kiswahili au Kiingereza kueleza unachohitaji. Anaweza kutafuta bidhaa na kupiga simu madukani kuulizia bei na upatikanaji wake, kisha kukuletea taarifa zinazokusaidia kuchagua pa kununua.
Kwa wasafiri, Kika anawezesha kutafuta na kukata tiketi za ndege, mabasi, SGR na boti kupitia WhatsApp. Pia anasaidia kutafuta hoteli kulingana na eneo, tarehe na bajeti yako, pamoja na kupata tiketi za mechi na matamasha kutoka kwa wauzaji rasmi.

Kwa wafanyabiashara, Kika anasaidia kuandaa ankara za awali na nukuu za bei zenye nembo ya biashara katika PDF. Pia anawezesha kufuatilia bidhaa zilizopo, madeni, matumizi na faida, huku taarifa zikionekana kwenye mfumo wa biashara.
Unaweza pia kumtumia picha au jina la dawa ili akusaidie kutafuta famasi yenye dawa hiyo karibu nawe. Huduma hii haichukui nafasi ya ushauri wa daktari.
Kuanza kutumia Kika ni bure kwa mgao wa awali wa tokeni vitengo vinavyotumika kupata huduma za AI. Zikiisha, unanunua nyingine; gharama za bidhaa na tiketi hulipwa kando.
📲 Rahisisha manunuzi, safari na shughuli za biashara yako leo! Tembelea https://kikapay.co.tz/ uanze kuzungumza na Kika kupitia WhatsApp.
