×

Video: Matonya Afunguka Alivyopanda Jukwaani Kufanya Shoo Akiwa Jela

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Matonya, amefunguka kuhusu maisha yake akiwa gerezani nchini Kenya, akisimulia changamoto alizokutana nazo pamoja na matukio mbalimbali yaliyotokea wakati akitumikia kifungo.

Katika mahojiano maalumu kwenye kipindi cha KONTENA, Matonya ameeleza kwa kina namna maisha ya gerezani yalivyokuwa, ikiwemo jinsi alivyowahi kufanya onyesho la muziki ndani ya gereza.

Mbali na simulizi hiyo iliyowavutia wengi, msanii huyo pia amezungumzia namna alivyokuwa akitekeleza ibada zake za kila siku, ikiwemo kwenda kuswali na mazingira ya msikiti aliokuwa akiutumia kwa ajili ya ibada.

Matonya amefunguka kuhusu kipindi hicho kigumu cha maisha yake alipokuwa akikabiliwa na matatizo ya kisheria nchini Kenya, akisimulia mambo mbalimbali aliyopitia akiwa mahabusu na gerezani.

Simulizi zake zimeibua picha ya maisha yake nje ya jukwaa, yakieleza upande mwingine wa safari ya mwanamuziki huyo mkongwe ambao mashabiki wengi huenda hawakuwahi kuufahamu.

Kupitia mahojiano hayo, Matonya ametoa fursa kwa mashabiki wake kufahamu zaidi changamoto alizopitia, namna alivyokabiliana nazo na matukio yaliyobaki kwenye kumbukumbu zake wakati wa kipindi hicho.

Leave a Comment