×

Rais Samia Ateua Makatibu Wakuu 7, Naibu Katibu 5, Msigwa Ahamishiwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na mabadiliko ya makatibu wakuu saba (7) na naibu makatibu wakuu watano (5) katika wizara mbalimbali za Serikali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Novemba 25, 2026, viongozi walioteuliwa na kupangiwa nafasi mpya ni kama ifuatavyo:

A. MAKATIBU WAKUU

  1. Agnes Meena – Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu. Awali alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Uvuvi.
  2. Prof. Mohammed Ali Sheikh – Katibu Mkuu wa Wizara ya Uvuvi. Awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Uvuvi anayeshughulikia masuala ya Uvuvi.
  3. Eliakim Chacha Maswi – Amehamishwa kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
  4. Gerson Partinus Msigwa – Amehamishwa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
  5. Abdallah Hassan Mitawi – Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi.
  6. Balozi Dkt. Samwel William Shelukindo – Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Awali alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  7. Charles Ngeleja Kadonya – Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki.

B. NAIBU MAKATIBU WAKUU

  1. Balozi Said Shaib Mussa – Amepangiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  2. Dkt. Fabian Magawa Madele – Amepangiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu. Awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Uvuvi anayeshughulikia masuala ya Miundombinu.
  3. Dadi Horace Kolimba – Amepangiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uvuvi. Awali alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
  4. Elijah Greenton Mwandumbya – Amehamishwa kutoka Wizara ya Fedha kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi.
  5. Dkt. Amos James Ibrahim – Am eteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha anayeshughulikia masuala ya Usimamizi wa Uchumi. Awali alikuwa Mhadhiri katika Chuo cha Kodi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uapisho wa makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu walioteuliwa utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

 

Leave a Comment