
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari – Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.
Uteuzi huo umetangazwa Novemba 25, 2026, kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, kuhusu mabadiliko ya muundo wa Wizara, uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali wa Serikali.
Kupitia uteuzi huo, Dkt. Rioba atashika nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari – Maelezo pamoja na kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, nafasi yenye jukumu la kuwasilisha na kutoa taarifa rasmi za Serikali kwa umma.
Uteuzi huo ni sehemu ya mabadiliko mbalimbali yaliyofanywa na Rais Samia katika nafasi za uongozi wa Serikali, yakihusisha mawaziri, manaibu mawaziri, makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu na viongozi wa taasisi za umma.
Taarifa hiyo imetolewa na Bakari S. Machumu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam.
