Stori: Mayasa Mariwata
MSANII anayefanya poa kwenye muziki, Mo Music amepingana na wasanii wenzake wanaoponda mabinti wa Bongo Muvi baada ya kuanika ukweli kwamba yupo ‘in love’ na binti mkali kutoka kwenye tasnia hiyo.
Akizungumzia maisha yake ya kimapenzi, Mo Music alisema kwenye mapenzi kila mtu ana mtazamo wake hivyo yeye ameona ni fresh kujiweka kwa msanii huyo bila kujali watu watasema nini.
“Hao wanaoongea acha waseme tu, mimi nina chombo changu matata cha Bongo Muvi, tena ni staa lakini hayo ya kusema sijui hawajatulia mimi naona huyu tunaelewana,” alisema Mo Music.